Sibuka FM
Sibuka FM
16 April 2025, 3:23 pm

“Tuna kila sababu ya kuupongeza uongozi wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa nanma ambayo umeweza kutekeleza dhana ya kumtua mama ndoo kichwani kwa vitendo na siyo kwa maneno leo hii maji safi na salama siyo swala la watu wachache kama ilivyokuwa hapo awali ama kweli mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni”.
Na, Daniel Manyanga
Imeelezwa kuwa jitihada zinazoendelea kufanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya maji, zimesaidia kuongeza upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wilayani Maswa kutoka asilimia 62.3 hadi asilimia 81 katika kipindi cha miaka minne hivyo kutekeleza dhana ya kumtua mama ndoo kichwani kwa vitendo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkurugenzi mtendaji wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Maswa (MAUWASA), mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa katika miaka minne ya Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mhe,Dkt.Samia Suluhu Hassan mamlaka hiyo imetekeleza na inaendelea kutekeleza miradi mbalimbali ili kuweza kufikia lengo la kuzalisha huduma ya maji safi na salama kwa wananchi ifikapo mwishoni mwa mwaka huu.
Katika hatua nyingine mkurugenzi mtendaji huyo wa MAUWASA, amesema kuwa maboresho ya huduma ya maji yanayoendelea kufanywa na serikali yameisaidia mamlaka hiyo kuweza kujiendesha yenyewe ikilinganishwa na hapo awali ambapo ilikuwa inaitegemea serikali kwa asilimia kubwa kuweza kujiendesha.
Kwa upande wao Janeth Martine na Mathayo Faustine wakazi wa wilaya ya Maswa wameeleza namna ambavyo utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji unaofanywa na serikali ulivyowaondolea changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama iliyokuwa ikiwakabili kipindi cha nyuma katika maeneo yao.
Mamlaka ya maji safi na usafiri wa mazingira mjini Maswa (MAUWASA) chini ya uongozi wa mhandisi,Nandi Mathias imeweza kuibuka kidedea kwa kuwa mamlaka ya kwanza kwa bora wa kutoa huduma katika mamlaka zilizopo chini ya EWURA huku wakiwa washindi wa tatu kwa mamlaka zote zilizopo Tanzania bara