Sibuka FM
Sibuka FM
14 April 2025, 12:56 pm

Katika Maeneo yote tuliyopita ya Mkoa wa Simiyu, Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mmeitendea haki Ilani ya ccm maana Miradi yote tuliyokagua ipo vizuri, Usimamizi Mzuri wa fedha unaonekana, kwakweli DC na DED Rais hakukosea kuwaleta hapa, Hongereni sana na timu yenu yote inayowasaidia kufanikisha haya. “Emmanuel Gungu Silanga MNEC Simiyu ”
Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi (ccm ) Mkoa wa Simiyu imeridhishwa na Utekelezaji wa Ilani ya ccm na Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa
Miradi iliyotembelewa ni mradi ya Kiwanda cha Chaki, Ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri, Jengo la Mionzi na kichomea taka katika Hospitali ya Wilaya, Ujenzi wa Bweni la Wasichana katika Shule ya Sekondari Salage na Ujenzi wa Jengo la Zahanati katika kijiji cha Mwamihanza
Wajumbe hao wakiongozwa na Emmanuel Gungu Silanga (MNEC) wameridhishwa na Usimamizi wa Fedha zinazotelewa na Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe, Dkt Samia Suluhu Hasani kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo
Akitoa taarifa kwa Wajumbe wa Kamati hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Maisha Mtipa, afisa Mipango wa Halmshauri hiyo Ndugu Julius Ikongora amesema kuwa Ujenzi wa Mradi wa Kiwanda cha chaki na Vifungashio umefikia asilimia 99 ukiwa umegarimu kiasi cha zaidi ya shilingi Bil 10

Eva Ndegeleki na John Makongoro ni wajumbe wa kamati ya Siasa ya chama cha Mapinduzi Mkoa wameshauri kipaombele cha ajira katika kiwanda cha chaki na Vifunganishio kizingatie wazawa wa maeneo husika hasa kwa kazi ambazo hazihitaji Ujuzi
Paul Jitula ni Mkazi wa Kijiji cha Nhami ambapo kiwanda hicho kimejengwa ameishukuru Serikali kwa Kujenga kiwanda katika Maeneo yao kwani kitaongeza ajira kwa Vijana na kuinua Uchumi

