Sibuka FM
Sibuka FM
13 April 2025, 1:31 pm

“Sisi wananchi wa Kitongoji cha Mnadani tumehamasika kupanda miti hasa kipindi hiki ambapo mvua zinaendelea kunyesha kwa sababu miti ina manufaa makubwa sana kwetu sisi binadamu pamoja na kulinda uoto wa asili wa ardhi yetu“
Wananchi wa Kitongoji cha Mnadani Kilichopo kata ya Nyalikungu Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamehamasika kupanda Miti katika Maeneo yanayozunguka Kitongoji hicho ili kurudisha uoto wa Asili na Utunzaji wa Mazingira.
Wakizungumza na Radio Sibuka Fm baadhi ya Wananchi hao wamesema kuwa wameamua kuwa na kampeni ya kupanda miti ili kuboresha Mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho na kupunguza hali ya Ukame
Wamesema kuwa Miti inafaida nyingi ikiwemo kuleta hali nzuri ya hewa, Vivuli majumbani, Kutengeneza Mbao, na kurudisha uoto wa Asili katika Ardhi
Anania Batungi ni mwenyekiti wa Kitongoji cha Mnadani amesema wameamua kuwa na kampeni hiyo katika kitongoji chake ili kuunga Mkono agizo la Serikali la kupanda miti hasa kipindi hiki cha Mvua huku akiomba Serikali iwape ushirikiano inapowakamata waharibufu wa Miti
