Sibuka FM

Maswa: Wananchi meno 32 nje baada yakufikiwa na mradi wa maji

20 March 2025, 6:03 pm

Pichani:Mwenye Skafu ni Mkuu wa Wilaya ya Itilima Bi,Anna Gidalya akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa maji Ipililo,pembeni yake mwenye kofia ni Wilson Magaigwa mratibu wa (CBWSO)Wilaya ya Maswa, akifuatiwa na Diwani wa viti maalumu,Bi,Modesta Kabeya na mwenye suti karibu yake ni katibu wa (Mb)Marko Bukwimba.Picha na Neema Solo

Serikali kupitia Wizara ya Maji imeendea na adhima yake ya kuhakikisha inamtua mwanamke ndoo kichwani kwakuhakikisha inasogeza  kuduma ya maji kwa wananchi.

Na,Alex Sayi-Maswa Simiyu

Wananchi na wakazi wa kijiji cha Ipililo kata ya Ipililo wilayani Maswa Mkoani Simiyu wameishukuru Serikali kwakuwasogezea huduma ya maji safi na salama.

Akizungumza na Sibuka fm wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi kwenye mradi wa maji kijijini hapo  Machi 19/2025 Diwani wa viti maalum Modesta Kabeya  amesema kuwa wanaishukuru Serikali kwakuwajali wakazi hao.

Sauti ya Modesta Kabeya Diwani viti maalum

Pelusi Goleka mkazi wa kijiji hicho amesema kuwa upatikanaji wa maji hayo utawaepusha wakazi hao kuepukana na magonjwa ya milipuko

Sauti ya Pelusi Goleka mkazi wa kijiji cha Ipililo

Kwa upande wake Salumu Zefania ameishukuru Serikali kwa kukamirika kwa mradi huo wa maji safi na salama kijijini hapo

Sauti ya Salum Zefania mkazi wa kijiji cha Ipililo

akisoma Taarifa ya utekelezaji wa mradi wa Maji kijijini hapo Mhandisi (RUWASA)Jofrey Kiama amesema kuwa mradi huo tayari umeshakamirika kwa 90% na unatarajia kuwahudumia wakazi zaidi ya elf,9

Sauti ya Mhandisi(RUWASA)Jofrey Kiama
Pichani:Ni kaimu meneja(RUWASA)Mhandisi Jofrey Kiama akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa maji.Picha na Neema Solo.

Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Itilima Bi,Anna Gidalya akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Maswa amesema kuwa kukamirika kwa mradi huu kunatokana na juhudi za Mbuge wa Jimbo hilo Mh,Stanslaus Nyongo.

Sauti ya Mkuu wa Wilaya Bi,Anna Gidalya
Pichani:Mkuu wa Wilaya ya Itilima Bi,Anna Gidalya akiwa kwenye chanzo cha maji.Picha na Neema Solo