Sibuka FM

Serikali kuimarisha kilimo cha pamba Simiyu

16 February 2025, 10:52 pm

Pichani wa kwanza kushoto ni Stanslaus Nyongo Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, akifuatiwa (katikati ) ni Mhe Kassim Majaliwa Waziri Mkuu wa Tanzania na (kulia kwake ) ni Mwenyekiti wa ccm Mkoa wa Simiyu Ndugu Shemsa Mohamed wakati wa Uwasilishaji wa Utekelezaji wa Ilani ya ccm 2020/2025 katika Jimbo la Maswa Mashariki

Na Nicholaus Machunda

Waziri  Mkuu  wa  Jamhuri  ya  Muungano  wa  Tanzania  na Mjumbe  wa   Kamati  Kuu ya  Halmashauri  Kuu ya  Taifa ya  Chama  Cha  Mapinduzi (CCM )  Mhe. Kassim  Majaliwa  amesema  kuwa  serikali  imejiimarisha  katika  kuinua  zao  la  pamba  ili  kuleta  tija  kwa  wakulima.

Mhe.  Majaliwa  amesema  hayo   wakati   akihutubia  wananchi  wa  Jimbo  la  Maswa   Mashariki  wakati  wa  uwasilishaji  wa  utekelezaji  wa  Ilani  ya  CCM  ya  mwaka 2020/2025 iliyofanyika  katika   uwanja  wa  Nguzo  Nane uliopo mjini  Maswa

Sauti ya Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Wilaya ya Maswa

Aidha  amesema  kuwa   lengo  la  Chama  Cha  Mapinduzi  na  serikali  ni  kujikita  kuboresha  huduma  za  afya  ili  upunguza  gharama  za  matibabu  kwa  wananchi ikiwemo wananchi  wa wilaya  ya  Maswa.

Sauti ya Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe Kassim Majaliwa akihutubia wananchi wa Maswa

Akitoa  taarifa  ya  utekelezaji  wa  Ilani  ya  CCM  ya  mwaka  2020/ 2025  Mbunge  wa  Jimbo  la  Maswa  Mashariki  Mhe   Stanslaus  Nyongo  amesema kuwa  fedha  nyingi  zimetolewa  na  serikali  kwa  ajili  ya   maendeleo katika  miradi  ya  maji,  viwanda, afya, elimu, kilimo na ufugaji

Sauti ya Stanslaus Nyongo Mbunge wa Maswa Mashariki akiwasilisha Utelezaji wa Ilani ya CCM
Baadhi ya wananchi waliojitokeza usikiliza uwasilishaji wa ilani ya CCM Maswa Mashariki

Shemsa  Mohamed  ni  Mwenyekiti  wa  Chama  Cha  Mapinduzi   Mkoa  wa  Simiyu  amewaomba  wananchi  wa  Wilaya  ya  Maswa  kumpa  Rais  zawadi  ya  kura   nyingi  za  ushindi  katika Uchaguzi  Mkuu utaokaofanyika Oktoba mwaka huu.

Shemsa  Mohamed – CCM