

5 February 2025, 5:06 pm
“Usalama wa raia na mali zake siyo jukumu pekee la jeshi la polisi nchini lakini tukishirikiana na jamii kwa ukaribu kupitia jeshi la jadi sungusungu tunaweza kumaliza vitendo vya kiahilifu katika maeneo yetu ya bila kutegemea hata jeshi la polisi waje watulinde ’’.
Na,Daniel Manyanga
Imeelezwa kuwa uwepo wa polisi jamii na ulinzi shirikishi katika maeneo mbalimbali mkoani Simiyu imesaidia kupunguza vitendo vya uhalifu na kuongeza ulinzi katika jamii tofauti na hapo mwanzoni .
Hayo yamesemwa na kaimu mkuu wa kitengo cha polisi jamii mkoa wa Simiyu Inspekta, Francis Msuku wakati akizungumza na Sibuka fm ofisini kwake na kueleza kuwa ushirikishwaji wa wananchi katika masuala ya ulinzi imesaidia kupunguza vitendo hivyo.
Nao baadhi ya wakazi wa mitaa mbalimbali mjini Bariadi wameeleza namna ambavyo polisi jamii na ulinzi shirikishi ulivyosaidia kupunguza vitendo vya kihalifu katika maeneo yao.