Sibuka FM

Mtoto wa miaka 3 afariki kwa kushambuliwa na Fisi Itilima

23 January 2025, 3:45 pm

Pichani ni muonekano wa mnyama Fisi akiwa katika mawindo ya kusaka chakula picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

‘‘Wanyamapori tunawahitaji sana hapa nchini kwa ajili ya utalii hali ambayo inaliingizia fedha za kigeni Taifa letu kupitia utalii kwa hifadhi zetu lakini hatuwezi kuwaacha kuwalinda watu wetu dhidi ya mashambulio ya wanyama pori wakali ambao wanatishia amani ya wananchi katika maeneo yao’’.

Na,Daniel Manyanga

Matukio ya fisi kuvamia na kushambulia watoto yameibuka tena mkoani Simiyu, baada ya miaka kadhaa iliyopita matukio hayo kuitikisa wilaya ya Bariadi ambapo kwa sasa matukio hayo yameshika kasi zaidi wilayani Itilima na katika kipindi cha miezi mitatu matukio hayo yamesababisha vifo vya watu nane, na tukio la hivi karibuni ni la kifo cha mtoto Saenda Kusendeka mwenye umri wa miaka mitatu ambaye alivamiwa na fisi majira ya jioni akiwa nyumbani na mama yake katika kijiji Mhunze wilayani Itilima hali iliyopelekea kifo cha mtoto huyo.

Kusengeka Saenda na Nsia Nindwa ni wanafamilia wa mtoto Saenda aliyefariki dunia kutokana na kushambuliwa na Fisi, na hapa wanaeleza mkasa huo ulivyokuwa hadi mtoto huyo kufariki dunia kutokana na shambulio hilo.

Sauti ya wanafamilia wa marehemu Saenda wakielezea namna ambavyo tukio la Fisi kuvamia na kuacha simanzi

Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu ACP. Edith Swebe amefika kijijini hapo na kuzungumza na wananchi, na kueleza jitihada za jeshi la polisi katika kudhibiti matukio ya wanyama wakali kuvamia na kushambulia wananchi hivyo kuacha maafa na makovu baadhi ya familia.

Sauti ya kamanda wa Polisi mkoa wa Simiyu,Edith Swebe akizungumza na wananchi baada ya kufika eneo la tukio
Kwenye picha aliyeketi kwenye kiti katikati ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Simiyu,ACP Edith Swebe (Chifu Nshoma) akiwa anasimikwa uchifu Picha kutoka maktaba ya Sibuka fm

Lawrence Okode ni kamanda wa uhifadhi wa  pori la akiba Maswa ambaye ameeleza hatua walizochukua hadi sasa baada na kabla ya tukio hilo la Fisi kuvamia na kushambulia mtoto hadi kifo chake.

Sauti ya mhifadhi wa pori la akiba Maswa akizungumza hatua ambazo wamezichukuwa tokea matukio hayo yaanze kujitokeza

Kwa upande mtemi wa sungusungu wa kijiji cha Mhunze, Mashini Malugu ameyahusisha matukio ya Fisi kushambulia na kuua watu na imani za kishirikina na kuiomba serikali kuwaacha watafute mwarobaini wao wenyewe utakaowasaidia kuliondosha tatizo hilo kijijini hapo.

Sauti ya kamanda wa Sungusungu akiomba serikali iwape ruhusu namna ya kushughulikia matukio hayo