DC Simalenga ataka uwazi ugawaji wa viuatilifu vya Pamba
17 January 2025, 8:14 pm
“Kilimo ni uti wa mgongo katika taifa letu ambapo zaidi ya asilimia 75 ya wananchi wake wanahusika na kilimo hivyo lazima tuwekeze nguvu kubwa ili kuzalisha kwa tija”.
Na, Daniel Manyanga
Mkuu wa wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu,Simon Simalenga amewataka viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika (AMCOS) wilayani humo kuwa waadilifu katika zoezi la ugawaji wa viuatilifu vya zao la pamba kwa wakulima, katika msimu huu wa kilimo wa mwaka 2024/2025.
Simalenga ametoa maelekezo hayo wakati akizungaumza na kipindi hichi ofisini kwake na kuwataka viongozi wa AMCOS kutohujumu zoezi la ugawaji wa viuatilifu hivyo pindi wakigawa.
Sylvanus Gwiboha ni mkuu wa divisheni ya Kilimo ,Mifugo na Uvuvi wa halmashauri ya mji wa Bariadi ameeleza mwenendo wa zoezi la ugawaji wa viuatilifu vya zao la pamba katika halmashauri hiyo.
Nao baadhi ya wakulima wa zao la pamba wilayani Bariadi wameiomba serikali kuharakisha zoezi la ugawaji wa viuatilifu hivyo ili waweze kupulizia pamba yao ambayo imeshaanza kushambuliwa na wadudu waharibifu katika zao hilo.