Wananchi Maswa wawekeana mikakati kumaliza Ugonjwa wa Kipindupindu
15 January 2025, 1:50 pm
Kwakweli inashangaza sana kuona watu hadi karne hii hawana vyoo na badala yake wanaenda kujisaidia Vichakani. ” Mrisho Mpoto balozi wa kampeni ya Mtu ni afya “
Wananchi wa kata za Sangamwalugesha, Malampaka na Shanwa zilizopo Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu wameweka mikakati ya kuhakikisha wanatokomeza Ugonjwa wa Kipindu pindu katika maneneo yao
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika Mikutano ya hadhara inayoratibiwa na Idara ya Afya kupitia kampeni ya “ Mtu ni afya” chini ya Balozi wa ampeni hiyo Mrisho Mpoto wamesema kuwa kutokomeza ugonjwa wa Kipindupindu inawezekana
Akitoa taarifa ya hali ya vyoo katika kata ya Malampaka , Mtendaji wa kata hiyo Jiyahile Gamaya amesema kuwa jumla ya kaya 37 hazina vyoo hivyo hupelekea kwenda kujisaidia polini na kuhatarisha afya za watu wengine
Kwa upande wake mwenyekiti wa Kijiji cha Sangamwalugesha ametoa maagizo kwa wananchi wake hasa kaya ambazo hazina choo kuhakikisha wanachimba na wale ambao hawana uwezo wa kuchimba watasaidiwa kupitia wajumbe wa Serikali yake ya kijiji.
Mrisho Mpoto ni Balozi wa kampeni ya Mtu ni afya amesema kuwa wanapokosa vyoo na kwenda kujisaidia vichakani wanachangia kusambaa kwa Ugonjwa wa Kipindupindu
Aidha Mpoto ameeleza hatua tano za kuzingatia katika Unawaji wa Mikono ili kujikinga na Ugonjwa wa kipindu pindu