Sibuka FM

Maswa:Viongozi wanawake watumikieni wananchi wote bila kujali itikadi za vyama vyao

10 December 2024, 11:37 am

Pichani ni kaimu katibu tawala wilaya ya Maswa , Emmanuel Saguda akizungumza na wanawake viongozi walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa na kuwataka kuwahudumia wananchi bila kujali itikadi za vyama vyao.

Uongozi ni dhamana ambayo umepewa na wananchi wenye imani na wewe hivyo ukipata nafasi jitahidi sana kuwa kioo kizuri kwenye jamii unayoiongoza ili siku moja uweze kukumbukwa kwa mazuri kutokana na utendaji kazi wako”.

Na, Daniel Manyanga

Wanawake viongozi walioshinda nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa serikali za mitaa uliofanyika mnamo tarehe 27.November.2024 wilayani Maswa mkoani Simiyu wametakiwa kuwatumia wananchi pasipo kujali vyama vyao ,ukabila,hali zao za maisha na udini ili kuleta maendeleo katika maeneo wanayoongoza.

Picha katika matukio zikionesha baadhi ya wanawake viongozi walioshinda nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa serikali za mitaa Picha na Daniel Manyanga

Wito huo umetolewa na kaimu katibu tawala wilaya ya Maswa , Emmanuel Saguda wakati wa hafra ya kuwapongeza wanawake hao waliothubutu kugombea nafasi mbalimbali na kushinda hafra iliyofanyika katika ukumbi mkubwa wa halmashauri hiyo.

Sauti ya kaimu katibu tawala wilaya ya Maswa, Emmanuel Saguda akiwataka wanawake hao kuwatumia wananchi katika maeneo Yao bila kujali utofauti wa vyama vyao.

Antonia Nkolela ni katibu wa umoja wa wanawake wa chama cha mapinduzi CCM (UWT) wilaya ya Maswa amesema kuwa kiongozi ni kioo cha jamii hivyo amewataka wanawake hao kusimamia masilahi ya wananchi.

Sauti ya katibu wa UWT wilaya ya Maswa, Antonia Nkolela akiwakumbusha majukumu ya uongozi katika maeneo wanayoongoza
Pichani ni katibu wa UWT wilaya ya Maswa , Antonia Nkolela akiwakumbusha majukumu ya uongozi

Awali akizungumza katika hafra hiyo mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Simiyu, Mwanahawa Saidi amesema kuwa lengo la hafra hiyo ni kuwapongeza wanawake viongozi kwa uthubutu wao wa kujitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi mkoani hapo na kuibuka washindi.

Sauti ya mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Simiyu, Mwanahawa Said akizungumza lengo la hafra hiyo ikiwa ni pamoja na kukumbushia wajibu wa kiongozi imara
Pichani ni mwenyekiti wa wanawake na Samia mkoa wa Simiyu,Mwanahawa Said akizungumza na wanawake viongozi hawapo pichani wakati wa hafra ya kuwapongeza kwa ushindi