DC Maswa awaita wananchi kwenye daftari la kudumu la wapiga kura
4 September 2024, 4:08 pm
“Uboreshaji wa taarifa katika daftari la kudumu la wapiga kura ni msingi mmoja wapo wa kupata viongozi bora kwa mustakabali wa Taifa letu hivyo ni muhimu kushiriki zoezi hilo.”
Na , Daniel Manyanga
Mkuu wa wilaya ya Maswa mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge ametoa wito kwa wananchi wilayani hapo kujitokeza Katika zoezi uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura lililoanza mnamo tarehe 04 mpaka September 10 mwaka huu Ili waweze kuwa na sifa za kushiriki uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu hapo mwakani.
Aswege Kaminyoge ametoa wito huo mapema leo hii alipotembelea baadhi ya vituo vinavyoandikisha kwa lengo la kujionea mwitikio wa wananchi na namna zoezi linavyoendeshwa katika halmashauri ya wilaya hiyo.
Aswege Kaminyoge ameyataka makundi ambayo yatahusika katika zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Katika hatua nyingine mkuu huyo wa wilaya ametoa agizo kwa viongozi wa serikali za mitaa kutoa taarifa za vifo kwa watu ambao walioandikishwa katika daftari la kudumu la wapiga kura mwaka 2019 ili waweze kuondolewa kwa majina yao katika daftari hilo kabla ya kuingia kwenye uchaguzi mkuu na serikali za mitaa.