Takukuru Simiyu ilivyorejesha Furaha ya Wananchi Wilayani Itilima
1 September 2024, 6:11 pm
Na Nicholaus Machunda
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Takukuru Mkoa wa Simiyu imefanikiwa kurejesha furaha ya Wananchi wa Wilaya Itilima baada ya kufuatilia Mradi wa Maji katika kijiji cha Ng’wang’wita uliotoa Huduma ya Maji kwa Mwezi mmoja tu baada ya kukamilika
Akitoa taarifa ya Utendaji kazi Robo ya nne ya Mwaka 2023/2024 Naibu Mkuu wa Takukuru Mkoa wa Simiyu Aron Misanga amesema kuwa Takukuru baada ya kubaini Mradi huo kushindwa kutoa huduma kama ilivyokusudiwa walifanya ufuatiliaji na kutoa Ushauri hatimae Mradi huo wa Maji ulianza kutoa Maji
Katika hatua ya Uchambuzi wa Mifumo Takukuru Mkoa ilifanya Uchambuzi katika Ukataji na Uwasilishaji wa Kodi ya Zuio (Withholding Tax ) na kubaini Halmashauri za Mkoa haliwasilishi Kodi ya zuio katika Mamlaka ya Mapato (TRA ) baada ya kuzikata kutoka kwa Watoa Huduma na Wazabuni
Aidha katika Program ya Takukuru RAFIKI Naibu Misanga amesema kuwa wamefanikiwa kufanya Vikao 70 katika Kata za Bariadi, Busega, Itilima, Maswa na Meatu na kupokea Kero Zaidi ya 500 kisha kuzitolea Mrejesho kwa Wananchi
Takukuru Mkoa wa Simiyu imesema kuwa kwa Kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba, 2024 itajielekeza zaidi katika Utoaji wa Elimu juu ya Mapambano dhidi ya Rushwa hasa tunapoelekea Uboreshaji wa Taarifa katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utaofanyika Mwishoni wa Mwezi Novemba, 2024