Sibuka FM

NEC: Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata wala kiapo Maswa

29 August 2024, 8:13 pm

Pichani:wa kwanza kulia ni Bi,Magdalena Rwebangira Mjumbe wa tume huru ya Taifa ya Uchaguzi,kulia kwake ni Afisa uandikishaji ngazi ya Jimbo Maswa Mashariki na Maswa Magharibi Maisha Mtipa nawa mwisho kulia ni Stanslaus Mukome Afisa tume huru ya Taifa ya Uchaguzi na (Mratibu Halmashauri ya Wilaya Maswa.)Picha na Alex Sayi.

Kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu 2025,Tume huru ya taifa ya uchaguzi imeendelea na zoezi la utoaji wa mafunzo kwa maafisa waandikishaji ngazi ya jimbo,maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya jimbo na maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya  kata kwa Mikoa ya Simiyu,Mara na Manyara.

Maafisa waandikishaji wasaidizi ngazi ya kata Wilayani Maswa Mkoani Simiyu hatimae rasmi wamekula kiapo cha usimamizi wa zoezi la uandikishaji kuelekea uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.

Maafisa hao wamekula kiapo hicho mbele ya Enos Slyvester Missana hakimu mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani hapa wakati wa mafunzo kwa maafisa hao yaliyofanyika kwenye ukumbu wa Halmashauri Wilayani hapa.

Missana akizungumza na maafisa hao amesema kuwa wanapaswa kukiheshimu kiapo hicho ili wasiweze kupatikana na makosa ya kisheria kwa kukiuka kiapo chao.

Pichani:wa kwanza kushoto mwenye Mic ni Hakimu mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani hapa Enos Missana,kushoto kwake ni stanslaus Mukome(Mratibu H/m ya Wilaya ya Maswa),akifuatiwa na Afisa mwaandikishaji msaidizi ngazi ya Jimbo Maswa Mashariki Vivian Christian,na mwenye simu ni Maisha Mtipa.Picha na Alex Sayi.
Sauti ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Maswa Mkoani hapa Enos Missana

Awali akifungua mafunzo kwa maafisa hao mgeni rasmi wa mafunzo hayo  na afisa uandikishaji ngazi ya jimbo Wilaya ya Maswa Mashariki na Maswa magharibi,Maisha Mtipa amewataka maafisa hao kusimamia kwa weredi utekelezaji wa zoezi hilo.

Pichani:Ni Maisha Mtipa Afisa mwaandikishaji ngazi ya Jimbo Maswa Mashariki na Maswa Magharibi.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Maisha Mtipa Afisa mwaandikishaji ngazi ya Jimbo Maswa Mashariki na Maswa Magharibi

Kwa upande wake Afisa Uhamiaji Wilayani hapa Constable Hashim Hamady,mbali yakutoa elimu ya Uraia kwa maafisa hao,lakini  pia aliwaasa  maafisa hao kutoa taarifa endapo watabaini uwepo wa raia wa kigeni wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo.

Pichani:Ni Afisa Uhamiaji Wilaya ya Maswa Mkoani hapa Constable Hashim Hamady.Picha na Alex Sayi
Sauti ya Afisa Uhamiaji Wilaya ya Maswa Mkoani hapa Constable Hashim Hamady

Aidha akitoa salamu za tume huru ya taifa ya uchaguzi mjumbe wa tume hiyo Bi,Magdalena Rwebangira amesema kuwa maafisa hao wa tume wanazungua kuhakikisha kuwa wanasimamia zaoezi hilo kikamirifu.

Sauti ya Bi,Magdalena Rwebangira Mjumbe wa tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.