Sibuka FM

NEC yawaomba wananchi Simiyu  kujitokeza kuboresha taarifa zao

26 August 2024, 5:19 pm

Picha ; Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Mhe Jaji Mstaafu Mbarouk S. Mbarouk katika Mkutano wa Tume na Wadau wa Uchaguzi kwenye Oboreshashaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu. Picha na Nicholaus Machunda

Tume huru ya uchaguzi imewataka wananchi mkoani simiyu kujitokeza kwa wingi kuboresha taarifa zao katika daftari la kudumu la wapiga kura, ili wawe na sifa za kushiriki uchaguzi ujao.

Akizungumza katika  Mkutano  huo   uliowakutanisha wadau mbalimbali mhe. Jaji mustaafu MBAROUK  S. MBAROUK  amewataka wananchi  Mkoani  Simiyu wajitokeze  katika zoezi hilo la uboreshaji  wa taarifa zao.

Sauti ya Makamu Mwenyekiti wa Tume Mhe Jaji Mstaafu Mbarouk Mbarouk

Naye Mwakilishi wa Mkurugenzi wa uchaguzi  Bw Selemani Mutabora akatoa takwimu za idadi ya matarajio kwa walio na sifa za kujiandikisha katika Daftari za Wapiga simiyu ikikadiliwa kuwa wapiga kura  wapya  Zaidi ya laki 1.4  ikiwa  ni  ongezeko  la  Asilimis 16  ya  Wapiga  kura  laki 9 walioandikishwa  awamu iliyopita  ya 2019/2020

Sauti ya Bw Selemani Mutabora

Kwa upande  wa Wadau walioshiriki katika mkutano huo ni pamoja na vyama vya siasa ambapo wamekili umuhimu   wao  katika kuhamasisha kupitia nafasi zao kama viongozi wa vyama mbalimbali.

Sauti za viongozi wa Siasa katika Kikao na Tume
Pichani Viongozi wa Vyama vya Siasa na Viongozi wa Dini wakifuatilia Mafunzo kutoka INEC

Aidha  katika  uzinduzi  huo Tume  imezingatia   makundi  maalumu  ikiwemo  Watu wenye  ulemavu wa aina  mbalimbali   huku  wakieleza changamoto za kimazingira katika maeneo na vituo vya kujiandishia.

Sauti za Viongozi wa Mahitaji Maalum wakati wa Mkutano na INEC

Kumalizika kwa mkutano huo kunaashiria kuanza rasmi kwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika mzunguko wan ne kwa mikoa ya simiyu, mara na manyara kwa kaulimbiu ya ‘kujiandikisha kuwa mpiga kura ni msingi wa kupata viongozi bora’ kajiandikishe sasa.

Baadhi ya Wawakilisha wa Mahitaji Maalum wakifuatilia Kikao na Tume