Wahandzabe Meatu wanavyotumia king’amuzi cha ndege pori kuipata asali
16 August 2024, 11:33 am
Wandzabe walia na Sheria za usimamizi wa wanyama pori na mapori tengefu kuwa zimechangia kuhafifisha usitawi wa jamii hizo na kusababisha hatari ya kutoweka kwa jamii hizo zinayoishi porini.
Na,Alex Sayi.
Jamii ya kihandzabe imebainisha kuwa kwa miaka nenda rudi imekuwa ikiwatumia Ndege pori kuwasaidia kubaini ilipo asali ambacho ni ndio chakula chao kikuu kwa jamii hiyo.
Hayo yamesemwa na Ezekieli Salamanda mkazi wa Makao Meatu Mkoani Simiyu ambae ni mhandzabe wakati akizungumza na Radio Sibuka fm,huku akibainisha kuwa wamekuwa wakiishi maisha yakutegemeana na viumbe hao.
Salamanda ameongeza kuwa wakiwa porini hukabiliwa na hatari nyingi ikiwemo kukabiliana na majoka yenye sumu kali lakini hulazimika kupambana ili kuhakikisha wanapata kitoweo.
Aidha kwa upande mwingine jamii hiyo imesema kuwa mabadiriko ya tabia ya Nchi yameendelea kuwaathiri kwakuwa kwa sasa jamii hiyo inaendelea kupoteza asili yake,mira na tamaduni zake.