Mil.163.5 zatumika ujenzi bweni la wasichana Mwagala
12 August 2024, 7:02 pm
Kufuatia uwepo wa changamoto zinazowakabili watoto wa kike Nchini za kushindwa kumaliza masomo yao kutokana na umbali wa Shule Serikali imendelea na Mpango wake wa kuhakikisha inajenga mabweni kwa ajili ya kuwanusuru watoto hao wa kike.
Na,Alex Sayi.
Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa Godfrey Eliakimu Mnzava amezindua nakuweka jiwe la msingi kwenye Bweni la wasichana Mwagala Sekondari lililopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu.
Bweni hilo lililopo kijiji cha Mwagala Kata ya Lalago Wilayani hapa limegharimu zaidi ya Shillingi Mil,163.9 huku kukamilika kwa Bweni hilo kukitajwa kusaidia kupunguza utoro na mimba zisizotarajiwa shuleni hapo.
Mkuu wa Shule hiyo Mwl,Jeremia Masolwa amesema kuwa kabla ya ujenzi wa Bweni hilo shule hiyo ilikuwa inakabiliwa na changamoto ya kukithiri kwa utoro na kukatisha masomo kwa sababu ya umbali wa shule hiyo.
Maria Marko mwanafunzi wa kidato cha pili Shuleni hapo amesema kuwa anaishukuru Serikali kwa kuwasaidia kuwajengea Bweni hilo ambalo litawasaidia kupata muda wakupumzika na kujisomea hali itayosaidia kuongeza ufaulu kwenye masomo yao.
Njile Ntungwa na Balinabas Masanja wazazi na wakazi wa Lalago wamezungumzia namna Bweni litakavyo wasaidia watoto hao wa kike kuepuka na changamoto zilizokuwa zikiwakwamisha nakushindwa kumaliza masomo yao.
Aidha Aswege Kaminyoge Mkuu wa Wilaya hiyo akitoa taarifa ya jumla amesema kuwa miradi (7) imepitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru nyenye thamani ya Shillingi Bil,4.7,kati ya Miradi hiyo Mwenge umezindua miradi(2)kuweka jiwe la msingi miradi(3)kutembelea,kuona nakukagua miradi(2)