Maswa wamshukuru Rais Samia kwa mradi wa maji Zanzui
9 August 2024, 7:26 pm
Na Nicholaus Machunda
Wananchi wa Vijiji vya Mabujiku, Malita na Zanzui vilivyopo kata ya Zanzui, Wilayani Maswa, Mkoani Simiyu wamemshukuru Mh Rais Samia Suluhu Hasani kwa kutoa Fedha kwa ajili ya Mradi wa maji utakaonufaisha Wakazi zaidi ya Elfu Tisa.
Wananchi hao wamesema kuwa kukamilika kwa Mradi huo utaenda kuondoa adha ya Upatikanaji wa maji katika Maeneo hayo licha ya Vijiji hivyo kuwa kwenye Chanzo cha Maji yanayotumika katika Mji wa Maswa na Vijiji 18 vinavyozunguka.
Akitoa taarifa ya Utekelezaji wa Mradi Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Maswa ( MAUWASA ) Mhandisi Nandi Mathias amesema kuwa Kukamilika kwa Madi huo utaongeza Upatikanaji wa Huduma ya Maji kutoka asilimia 78 hadi kufikia asilimia 95
Mashimba Ndaki ni Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi ambapo Mradi huo unatekelezwaa amesema kuwa anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hasani kwa kutoa fedha nyingi katika Jimbo lake na kutekeleza azma ya kumtua mama ndoo kichwani
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2024 Godfrey Eliakimu Mzava amewapongeza MAUWASA kwa kutekeleza maono ya Rais kwa Vitendo na kuwataka wananchi wa Wilaya ya Maswa kujitokeza kwa Wingi kushiriki nafasi mbalimbali za Uongozk katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika mwishoni mwa Mwaka huu.