Shimo lakatisha maisha ya Anna, Martha Bariadi
19 July 2024, 2:27 pm
“Usalama wa maisha ni jambo muhimu ili kutimiza malengo ya wananchi wetu nchi bila kuhakikisha usalama wa maeneo wanapotoka wananchi hatuwezi kufikia azma ya maendeleo ngazi ya jamii na taifa kwa ujumla”
Na Daniel Manyanga
Wanafunzi wawili waliotambulika kwa majina ya Anna Mayunga (14) na Martha Dickson (13) wanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi Mahaha kata ya Bunamhala wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamefariki dunia baada ya kutumbukia kwenye dimbwi la maji lililopo kandokando ya barabara ambalo lilichimbwa kwa ajili ya kuchotea molam kwa ajili ya ujenzi wa barabara.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Simon Simalenga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo baada ya kufika shuleni hapo na eneo la tukio na kisha kutoa maelekezo ya uchunguzi kufanyika juu ya tukio hilo.
Charles Yamungu ni mmoja wa walimu wa shule ya msingi Mahaha ambaye anaeleza ni kwa namna gani watoto hao walitoka shuleni na kwenda katika dimbwi hilo.
Kwa upande wao baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo na mmoja wa ndugu wa marehemu wameeleza tukio hilo lilivyotokea.