Sibuka FM

Maswa:Wananchi wa Zanzui meno thelathini na mbili nje mradi wa maji safi

17 July 2024, 9:45 pm

Pichani ni mbunge wa jimbo la Maswa magharibi,Mhe Mashimba Ndaki picha kutoka maktaba ya Sibuka Fm

Katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za kijamii serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania awamu ya sita imeendelea kutekeleza adhima  ya kumtua Mama ndoo kichwani kwa vitendo”

Na, Daniel Manyanga  

Zaidi  ya billion 1.5 zinatarajiwa kutumika kupeleka huduma ya maji safi na salama kwa wananchi wa kata ya Zanzui wilayani Maswa mkoani Simiyu ili kutimiza adhima ya serikali ya awamu ya sita ya kumtua Mama ndoo kichwani.

Hayo yamesemwa na mbunge wa jimbo la Maswa magharibi ,Mashimba Ndaki wakati wa mkutano wa hadhara na wananchi katani hapo wa  kusikiliza kero mbalimbali na kuzitafutia ufumbuzi ikiwemo na kuangalia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa mwaka 2020 ya Chama Cha mapinduzi CCM kwa wananchi wake.

Mashimba Ndaki amesema kuwa katika kutimiza malengo ya serikali ya awamu ya sita ya kupeleka huduma za kijamii kwa wananchi Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha fedha billion 1.52 ili kupeleka huduma ya maji kwa wananchi wa kata ya Zanzui ambao walikuwa hawana maji safi na salama licha ya kwamba katani hapo kuna bwawa la Zanzui linalohudumia mji wa Maswa na vijiji 20 kupitia mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Maswa MAUWASA .

Sauti ya mbunge wa jimbo la Maswa magharibi, Mashimba Ndaki akielezea mapokeo ya mradi wa maji.
Pichani ni muonekano wa Tanki la maji likiwa linajengwa ili kuhifadhia maji

Mashimba Ndaki amemshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kukubali ombi lake la fedha za mradi wa maji kwa wananchi huku akiwaomba wananchi wataofanikiwa kuvuta maji kwenye makazi yao kutunza miundombinu ili iweze kudumu kwa muda mrefu kwa matumizi ya vizazi vingine.

Nao baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo wamepongeza juhudi za mbunge huyo katika kupigania na kutimiza ahadi zake ambazo aliahidi wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2020 hivyo wameahidi kufanya vyema ikifika wakati wa uchaguzi mkuu hapo mwakani.

Sauti ya Mashimba Ndaki na Wananchi wakipongeza kuhudi za serikali za kusogeza huduma za kijamii karibu