Nyongo amwaga maua kwa Dkt.Samia kwa utekelezaji miradi Maswa
11 July 2024, 4:49 pm
“Ujenzi wa mabweni mashuleni watajwa kuwa mwarobaini wa kukabiliana na mimba mashuleni haswa kwa wanafunzi wa kike Ili waweze kutimiza malengo yao”
Na, Daniel Manyanga
Naibu waziri ofisi ya Rais mipango na uwekezaji ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Maswa mashariki Mhe.Stanslaus Nyongo amesema serikali imepanga kujenga mabweni kwa shule zote za sekondari jimboni hapo ili kumlinda mwanafunzi wa kike na vishawishi kutoka kwa Wanaume ili kuweza kutimiza malengo.
Stanslaus Nyongo amesema hayo wakati wa ziara ya kikazi jimboni hapo ya kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kupitia fedha zinazotolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan akiambatana viongozi wakuu ngazi ya wilaya na wakuu wa idara ili kujionea namna ambavyo wananchi wanaweza kunufaika na utekelezaji wa miradi hiyo.
Nyongo amesema kuwa ili kutimiza malengo ya wanafunzi wa kike wanaosoma masomo ya sekondari serikali imejipanga kujenga mabweni ili kuwalinda na vishawishi vya wanaume hali ambayo inapelekea wengi wao kushindwa kuhitimu masomo yao baada ya kupata ujauzito wakiwa shuleni.
Naibu waziri ofisi ya Rais mipango na uwekezaji, Stanslaus Nyongo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha nyingi katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo wilayani Maswa huku akiahidi kusimamia miradi hiyo ili iweze kuleta tija kwa Wananchi wilayani hapo.