Wananchi wilayani Meatu wachangia maji na ng’ombe
10 July 2024, 1:03 pm
“Maji ni uhai kwa binadamu lakini wananchi wa wilaya ya Meatu wapo hatarini kupata magonjwa yatokanayo na kutumia maji ya visima na mabwawa wao pamoja na mifugo ’’
Na,Daniel Manyanga
Wakazi wa kata ya Mwandoya wilayani Meatu, mkoani Simiyu wameiomba serikali kuwasaidia kuondokana na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama wanayoipitia kwa sasa ambapo wanalazimika kutumia maji ya visima na mabwawa kwa kuchangia na mifugo inayotumia maji ya bwawani hali inayohataraisha usalama wa afya zao.
Wakizungumza mbele ya mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe.Kenani Kihongosi wakati wa mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi ambapo wananchi hao wakapaza sauti kwa mkuu wa mkoa kutokana na magumu wanayopitia ya kuchangia maji na mifugo.
Awali kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Meatu mhandisi Bruno Paul amezitaja changamoto zinazosababisha huduma ya maji kutokuwa ya uhakika katika Kata ya Mwandoya.
Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Simiyu, Mhe.Kenani Kihongosi ametoa maelekezo kwa wakala wa maji safi na usafi wa mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Meatu kuongeza ufanisi na kuhakikisha wananchi wanapata maji safi na salama ili kuepusha magonjwa yanayoweza kutokana na kutumia maji machafu.