Tamasha la utalii, utamaduni Kanda ya Ziwa lazinduliwa Simiyu
6 July 2024, 9:56 am
Kila kabila wana utamaduni wao, wasukuma wana utamaduni wao pia, ni vema kila kabila likaenzi utamaduni wake unasaidia katika Kulinda maadili na kukuza uchumi wa Taifa kupitia Utalii “Dunstan Kitandula ” Naibu waziri wa Maliasili na Utalii
Tamasha la Utali na Utamaduni Kanda ya Ziwa limezinduliwa rasmi Wilayani Bariadi Mkoani Simiyu likiwa na lengo la kudumisha na kuenzi Mila, tamaduni na Desturi za kabila la Wasukuma
Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tamasha hilo Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe Dunstan Kitandula amesema ni Muhimu kuenzi tamaduni zetu na kuchochea ukuaji wa Uchumi kupitia utalii.
Magesa Nyambeho ni Afisa Utamaduni Mwandamizi kutoka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kumekuwepo na Mmomonyoko wa Maadili katika Jamii hivyo Serikali imeandaa muongozo wa Maadili kwa Wasanii ambao ndio imekuwa kichocheo kikubwa.
Kwa Upande wa Wandaaji wa Tamasha hilo Kilimanjaro One Tour and Travel kupitia kwa Mkurugenzi Mtendaji Bi Christina Jengo amesema kuwa Tamasha hilo limelenga kukuza Utamaduni wa Kabila la Wasukuma .
Naye Mwenyekiti wa Utamaduni Mkoa wa Simiyu Buhimila Shala amesema kuwa ni vyema watu wakajua Utamaduni wa Kisukuma siyo Uchawi na kuiomba Serikali iwaunge Mkono katika kuendeleza na Kuenzi Mila na Utamaduni wetu.
Tamasha la Utamaduni Kanda ya Ziwa limezinduliwa rasmi katika Viwanja vya ccm wilayani Bariadi tarehe 05. 07. 2024 na litakuwepo kwa Muda wa Siku tatu ambapo kilele chake ni Tarehe 07. 07. 2024