Sibuka FM

RC  Kihongosi  aangiza Miradi ya RUWASA  Simiyu Kukamilishwa  kwa Wakati

4 July 2024, 10:37 am

Pichani aliyesimama ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh Kenan Kihongosi, wa pili kulia kwake (mwenye Koti Jeusi ) Mhandisi Emmanuel Luswetula Kaimu Meneja RUWASA Mkoa wa Simiyu akifuatiwa na meneja RUWASA Wilaya ya Maswa (mwenye Miwani) Mhandisi Lucas Madaha Wakati wa Kikao kazi cha RUWASA. Picha na Nicholaus Machunda

Niwapongeze sana RUWASA Mkoa wa Simiyu kwa kazi kubwa mnayofanya ya kumheshimisha Mhe Rais Samia, kwakweli Sekta ya Maji imekuwa na Mageuzi makubwa sana, Niwaombe Mtekeleze miradi kwa Wakati na kwa Ubora ili Wananchi waweze kunufaika ” RC Kihongosi “

Mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu  Mhe,  Kenani  Laban  Kihongosi  ameiagiza  Wakala  wa  Maji  na  Usafi  wa  Mazingira  Vijijini – RUWASA  Mkoa  wa Simiyu  kuhakikisha  Miradi  wanayotekeleza  kukamilika  kwa  Wakati  na  kwa  Ubora  ili  iweze  kunufaisha  wananchi.

Mhe  Kihongozi  ametoa  maagizo  hayo  katika  kikao  Kazi  cha  Mwaka   cha  RUWASA  kilichofanyika  Wilayani   Busega  na  kusema  kuwa   Watanzania  wanawategemea   katika  Upatikanaji  wa  Huduma  ya  Maji   hivyo  wana dhamana  kubwa    huku  akizitaka  taasisi  zote  za Serikali zinazodaiwa  bili za  Maji  kulipa.

Hii hapa ni sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi

Aidha  Mkuu  wa  Mkoa  amewapongeza    Watumishi  wa  Ruwasa   kwa  kazi  kubwa  wanayofanya  ya  kuwahudumia  wananchi  katika  Sekta  ya  Maji  kwani kumekuwa  na  Mageuzi  makubwa  katika  Sekta  hiyo  na  kuendana  na  kauli  ya   Rais  ya  Kumtua  Mama  ndoo  kichwani

Hii hapa ni sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenani Kihongosi

Akitoa  taarifa  kwa  Mkuu  wa  Mkoa ambaye alikuwa  Mgeni  Rasmi  katika  Kikao  kazi  hicho,  Kaimu Meneja  wa  RUWASA  Mkoa  wa  Simiyu  Mhandisi   Emmanuel  Luswetula   amesema  kuwa  hadi  kufika  mwezi  june  mwaka  huu  2024  Wastani  wa  upatikanaji  wa  huduma  ya  Maji  umefikia  Asilimia  70.

Sauti ya Mhandisi Emmanuel Luswetula -Kaimu Meneja Ruwasa Mkoa wa Simiyu

Mhandisi  Lucas  Madaha  Meneja  Ruwasa  Wilaya  ya  Maswa,  Mhandisi  Nusra   Msoke  Kaimu  Meneja  Ruwasa  Wilaya  ya  Bariadi na  Mhandisi  Daniel  Gagala  Meneja Ruwasa Wilaya ya  Busega Wanaeleza  namna  wanavyotekeleza  Miradi  katika  Wilaya   na   Mikakati  yao  ili  kufikia   Asilimia  76  ifikapo  Desemba, 2024

Sauti ya Meneja Ruwasa Wilaya ya Maswa, Bariadi na Busega wakielezea Mipango yao
Watumishi wa Ruwasa wakifuatilia kikao
Watumishi wa Ruwasa wakifuatilia kikao