MAUWASA yataja sababu za maji kutokuwa angavu
28 June 2024, 10:07 pm
Kutokana na wingi wa mvua zilizonyesha kwa mwaka huu imepelekea bwawa letu la New Sola kuwa na magugumaji mengi pamoja na shughuli za kibinadamu zinazofanyika zimesababisha maji kutokuwa angavu ” Kasimu Kado “
Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Mjini Maswa (MAUWASA ) imesema kuwa sababu kubwa ya Maji kutokuwa ang’avu ni kutokana na kuwepo kwa MaguguMaji pamoja shughuli za kibinadamu zinazofanya kando ya Bwawa la New Sola maarufu kwa jina la Bwawa la Zanzui
Akizungumza na Waandishi wa Habari , Kaimu Mkurugenzi wa MAUWASA Kasimu Abdallah Kado amesema kuwa Mamlaka imeanza Zoezi la kusafisha MaguguMaji katika Bwawa hilo ili wananchi waendelee kupata Maji Safi na Salama.
Kaimu Mkurugezi huyo ametoa Wito kwa Wananchi kuwa na Subira wakati zoezi hilo likiendelea kufanyika na kusisitiza Wananchi wanaozunguka Bwawa hilo kuendelea kutunza vyanzo vya Maji ili visaidie Vizazi vya Sasa na Vijavyo
Aidha amewataka Wafugaji kutopeleka Mifugo yao katika Bwawa na Badala yake wapeleke kwenye Vituo vilivyotengwa kwa ajili ya Kunyweshea maji Mifugo yao