Sibuka FM

Warina asali wateketeza madarasa manne kwa moto Bariadi

28 June 2024, 10:43 am

Pichani ni Kaimu Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Simiyu, ASF Faustine Mtitu. Picha kutoka maktaba ya Sibuka FM

Elimu ya kujikinga na majanga kwa jamii inahitajika sana ili kusaidia kupunguza matukio ya moto hasa kwenye taasisi za umma na binafsi matukio ambayo yanatokea kwenye jamii zetu lakini inakosekana elimu ya kuzuia hayo majanga.”

Na, Daniel Manyanga 

Watu wasiojulikana waliokuwa wanarina asali wameteketeza kwa moto madarasa manne katika shule ya msingi Kidinda iliyopo halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu  usiku wa kuamikia June 27,2024 kufuatia kulina  asali iliyokuwa kwenye dari ya veranda ya mbele ya madarasa kwa kutumia moto.

Hayo yamesemwa na kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu mrakibu msaidizi,Faustine Mtitu baada ya kufika eneo la tukio ambapo amesema kuwa sababu kubwa ya kuteketea kwa moto madarasa hayo ni watu wasiojulikana waliokuwa wakilina asali katika darasa moja wapo kwa kutumia moto kwenye jengo hilo ambalo lilikuwa halina hata umeme.

Sauti ya kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji akizungumza kwenye tukio la moto kwa madarasa manne.

Adrian Jungu ni mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Bariadi amesema kuwa tayari jeshi la polisi linamshikilia mlinzi wa shule hiyo ili kulisaidia jeshi la polisi kwenye uchunguzi juu ya tukio lililotokea mapema usiku majira ya saa nne.

Sauti ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya mji wa Bariadi , Adrian Jungu akielezea hatua zilizochukuliwa

Kwa upande wake,Samora Kakuba na Reuben Masali ni baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wametoa wito kwa wananchi katika maeneo wanayoishi kuwa na ushirikiano katika swala la ulinzi wa mali za umma huku wakiomba serikali kuwachukulia hatua kali za kisheria wale wote waliohusika na tukio hilo.

Sauti ya baadhi ya mashuhuda wa tukio wakielezea jinsi walivyoona

Katika hatua nyingine kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Simiyu Mrakibu msaidizi,Faustine Mtitu ametoa wito kwa jamii katika kukabiliana na matukio ya moto mkoani hapo.

Sauti ya kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji akitoa wito