Sibuka FM

Wadau wa maji Maswa wajadili uboreshaji wa huduma ya maji vijijini

24 June 2024, 1:07 pm

Pichani (aliyesimama) Meneja RUWASA Wilaya ya Maswa Mhandisi Lucas Madaha

Serikali imeleta fedha nyingi za miradi ya maji vijijini lakini mwitikio wa wananchi kutumia maji ya bomba ambayo ni safi na salama ni mdogo sana na badala yake wanatumia maji ya madimbwi ambayo siyo safi na salama hali inayopelekea kuwavunja moyo wanaoleta fedha hizo.

Wadau  wa  maji wilayani  Maswa mkoa wa Simiyu wamejadili  namna ya uboreshaji  wa huduma ya  maji  vijjijini   chini  ya  Wakala  wa  Maji  na  Usafi  wa  Mazingira  Vijijini –RUWASA

Akifungua  kikao  hicho  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe,  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  derikali  imetenga  fedha  kwa  ajili  ya  vijiji  ambavyo  vina changamoto  ya  maji ili navyo vipate maji.

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge wakati wa kikao cha Wadau wa Maji

Mhe   Kaminyoge  amesema serikali  imetoa  fedha  nyingi  kwa  ajili  ya maji  hivyo inategemea  kuona  matokeo ya mabadiliko katika huduma ya maji huku  akiwapongeza Wakala  wa  Maji  na  Usafi  wa  Mazingira  Vijijini – RUWASA  Wilaya  ya  Maswa  kwa  kazi  nzuri  wanayoifanya  ya  kuleta  huduma  ya maji.

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge
Pichani Wadau wa Maji Wilayani Maswa Wakifuatilia kikao

Meneja  RUWASA   Wilaya  ya  Maswa  Mhandisi  Lucas  Madaha  amesema  kuwa  katika  mwaka huu  wa fedha ipo miradi wanayoendelea  kuikamilisha  ili kuhakikisha wanatekeleza  kampeni  ya  kumtua  mama ndoo kichwa.

Sauti ya Meneja RUWASA Mhandisi Lucas Madaha

Aidha  Mhandisi  Madaha  amesema  kuwa  kwa  mwaka ujao RUWASA Wilaya ya Maswa imejipanga  kuongeza upatikanaji  wa huduma ya maji na  kukamilisha  miradi  ambayo  haijakamilika   kwa  mwaka unaoisha.

Sauti ya Meneja RUWASA Mhandisi Lucas Madaha wakati wa kikao cha Maji

Kwa  uapande  wake   Afisa  Maendeleo  ya  Jamii  wa Ruwasa  Willison   Magaigwa  amesema  kuwa  licha  ya  Serikali  kupeleka  miradi  ya  Maji  bado  mwitikio  ni  Mdogo  wa  Wananchi  kutumia  Maji  ya  Bomba  ambayo  ni  Safi  na  Salama

Sauti ya Willison Magaigwa Afisa Maendeleo RUWASA Maswa

Baadhi  ya  Madiwani  waliohudhuria  Kikao  hicho  cha  Wadau  wa  Maji  wamehoji  kuwa  ni  vigezo gani  vinavyotumika  kubaini  changamoto  za  Maji  kwenye  Vijiji  na  watu  gani  wanaowashirikisha  katika  kubaini  changamoto  hizo.

Sauti za Madiwani wakichangia wakati wa kikao cha wadau wa Maji
Wadau wa Maji wakifuatilia maelezo ya Meneja wa RUWASA Maswa Lucas Madaha aliyesimama Mbele