Sibuka FM

RC Kihongosi aagiza kurejeshwa  fedha  za mikopo ya vikundi Maswa

24 June 2024, 12:33 pm

Pichani (aliyesimama )Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Kenan Kihongosi akiongea wakati wa Baraza la kupitia Hoja za CAG katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe, Kenan Kihongozi ameahidi kuunda tume ya kufuatilia urejeshaji wa mikopo ya 10% kwa vikundi vya wanawake, vijana na makundi maalum inayotolewa na halmashauri ili watanzania wengine waweze kukopa.

Mkuu  wa  Mkoa  wa  Simiyu  Mhe   Kenan   Laban  Kihongosi   amemwagiza  Mkurugenzi  Mtendaji wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa kuhakikisha  wote waliochukua  Mikopo ya Asilimia  Kumi (10%) inayotolewa  kwa Vikundi  vya  Wanawake, Vijana  na  Makundi  Maalumu   warudishe  ili  Watanzania  wengine  waweze  kukopa.

Mhe  Kihongosi  ametoa  maagizo  hayo  Wilayani  Maswa  wakati  wa  Kikao  cha  Baraza  la  Madiwani  la kujadili  Hoja  za  Mkaguzi  na Mdhibiti wa  Hesabu  za  Serikali ( CAG ) na  kusema  kuwa  ataunda  tume  maalumu  kwa  ajili  ya  kufuatilia   urejeshaji  wa   Mikopo  hiyo  ili ziweze  kunufaisha  wengine

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe, Kenan Kihongosi

Aidha  Mkuu  wa  Mkoa  ameipongeza   Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  kwa  kupata  HATI  Safi  ya  Ukaguzi  wa  Hesabu  za  Serikali  huku  akiwata kuwachukulia  hatua   wote  waliosababisha  Hoja  kwa  Uzembe  wa  Makusudi  ili  Watanzania  waendelee  kuiamini  Serikali  yao.

Sauti ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe, Kenan Kihongosi

Akitoa  taarifa  za  Ukaguzi  wa  Hesabu  za  Serikali,  kwa  niaba  ya  Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  ya Wilaya ya  Maswa,  Mweka  Hazina  wa  Halmashauri hiyo   Lwiza  Sudi   amesema  kuwa  Hoja iliibuliwa  kutokana  na  Deni  la  Mkopo  wa  Asilimia  kumi  (10% ) unaotolewa  kwa  Vikundi  vya Wanawake, Vijana  na  Watu  wenye  Ulemavu kutorejeshwa.

Sauti ya Lwiza Sudi – Mweka hazina Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Kwa  Upande  wake  Mkuu  wa  Wilaya  ya  Maswa  Mhe,  Aswege  Kaminyoge  amesema  kuwa  anamshukuru  Rais  Samia  kwa  kutoa  Fedha  nyingi  kwa  ajili  ya  Miradi mbalimbali  ya  Maendeleo  kwa  Wananchi   wa  Maswa  .

Sauti ya DC Maswa Mhe, Aswege Kaminyoge wakati wa baraza la Hoja za CAG
Pichani ni Madiwani wa Halmashauri ya Maswa wakifuatilia kikao cha Baraza la Hoja za CAG

Jeremia  Shigala  na  Aron  Mboje  ni   Madiwani  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa   wamemshukuru  Mkuu  wa  Mkoa  kwa  kuwapitisha  vyema  katika  Hoja  za  CAG  na  kuahidi  kuyasimamia  na  kuyafanyika  kazi   ili  Halmashauri  iendelee  kupata  HATI  safi.

Sauti za Baadhi ya Madiwani wakichangia Hoja wakati wa Baraza la Hoja CAG