Watembea umbali wa kilomita 35 kufuata huduma za TRA mjini Maswa
10 June 2024, 5:47 pm
“Tunaomba sana elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara itolewe kwa upana wake na mara kwa mara ili tuweze kulipa kodi kwa hiari hali itakayoweza kujenga urafiki na TRA.”
Na, Daniel Manyanga
Wafanyabiarasha wa Mji mdogo Malampaka wilayani Maswa mkoani Simiyu waomba kusogezewa kwa huduma za mamlaka ya mapato nchini(TRA)ili kupunguza gharama za kufuata huduma za ulipaji kodi kwa hiari.
Wafanyabiashara hao wameyasema hayo wakati wa kikao cha pamoja kilichoandaliwa na (TRA) kwa lengo la kutoa elimu ya mlipa kodi kwa hiari kilichofanyika ukumbi wa Ntuzu uliopo mjini Malampaka.
Akizungumza na Sibuka fm,Noel Shigolo katibu wa umoja wa wafanya biashara mjini Malampaka amesema kuwa umbali wa ofisi za (TRA) ambao ni zaidi ya Km,35 unachangia kuchelewa kulipa kodi kwa wakati kwa baadhi ya wafanyabiashara.
Martine Kamzora mkazi na mfanyabiashara wa Malampaka amewashukuru maafisa wa(TRA) kwa kuona umuhimu wa kukutana na wafanyabiashara nakuweza kusikiliza kero zao zinazowafanya kukwepa au kushindwa kulipa kodi kwa wakati.
Kwa upande wake ,Issack Mathayo afisa msimamizi wa kodi wilayani hapa amesema kuwa wamelazimika kuwafikia wafanya biashara hao nakuwapa elimu ya ulipaji kodi hali itakayosaidia kuongeza uhiari wa wafanyabiashara hao wa kulipa kodi.
Mathayo amekili changamoto ya umbali unaochangia baadhi ya wafanyabiashara wa mji mdogo wa Malampaka kuchelewa au kushindwa kulipa kodi kwa wakati.