Sibuka FM

RC Nawanda aagiza halmashauri kutenga bajeti ya michezo mashuleni

31 May 2024, 7:16 pm

Pichani ni mkuu wa wilaya ya Maswa, Aswege Kaminyoge akikabidhi mpira kwa mwanafunzi wa mahitaji maalumu Picha ni kutoka ofisi ya RC

Utengaji wa bajeti ya ununuzi wa vifaa vya michezo mashuleni utaongeza wanamichezo hivyo kutengeneza ajira nyingi na kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

Na.Daniel Manyanga 

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda ameziagiza halmashauri zote mkoani hapo kutenga fedha za  ununuzi wa vifaa vya michezo mashuleni na uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA na  UMISSETA.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Maswa , Aswege Kaminyoge aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt.Yahaya Nawanda kwenye ufunguzi wa michezo ya wanafunzi wa shule za msingi ngazi ya mkoa UMITASHUMTA katika shule ya sekondari ya wasichana ya Maswa girls.

Aswege Kaminyoge amesema kuwa michezo ni ajira ambayo inalipa pesa nyingi hivyo halmashauri zitengeneze mazingira mazuri kwa wanamichezo ili kuweza kukuza vipaji vyao kuanzia mashuleni hadi kitaifa kwa kutenga bajeti ya ununuzi wa vifaa vya michezo pamoja uendeshaji wa michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA kitaifa.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akitoa maagizo kwa halmashauri kutenga fedha za michezo

Aswege Kaminyoge amewataka wanamichezo watakaochaguliwa kwenye timu ya mkoa itakayoenda kuwakilisha kitaifa mkoani Tabora kuwa na nidhamu wawapo kambini na kule mkoani Tabora pamoja na kujituma wakati wote wa mashindano huku maafisa elimu,michezo na utamaduni wakitakiwa kushirikiana kwa pamoja ili kujenga uelewa wa michezo mashuleni.

Sauti ya mkuu wa wilaya ya Maswa akitoa maagizo kwa wasimamizi wa michezo

Awali mwakilishi wa afisa elimu mkoa wa Simiyu,Mwl Esther Marwa ametaja michezo watakayoshiriki hivyo amewaomba wanafunzi waliochaguliwa kambini kuwa na nidhamu na kudumisha usafi wakati wote wa michezo.

Sauti ya mwakilishi wa afisa elimu mkoa Mwl Esther Marwa