Maswa kuchanja ng’ombe zaidi ya laki 2
26 May 2024, 10:27 am
Zoezi la chanjo ya mifugo ni muhimu sana kwa wafugaji hivyo kila diwani akawe balozi kwenye eneo lake ili kuhamasisha waitikie kuchanja Mifugo yao ili kujikinga na Ugonjwa wa Mapafu “Maisha Mtipa Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Maswa”
Halmashauri ya Wilaya ya Maswa mkoani Simiyu inatarajia kuchanja ng’ombe 244, 512 ili kujikinga na ugonjwa wa mapafu unaohatarisha afya ya mifugo hiyo.
Akitoa taarifa kwa Baraza la Madiwani robo ya tatu ya Mwaka wa Fedha 2023/ 2024 kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri, Mkuu wa Division ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Wilayani hapa Robert Urasa amesema lengo la chanjo hiyo ni kudhibiti Magonjwa ya Mifugo
Sylvanus Mipawa ni Diwani wa Kata ya Buchambi na Petro Ng’wandu Diwani wa kata ya Mwamanenge wamesema zoezi hilo laziwa lipewe kipaombele ili kunusuru Mifugo ya Wafugaji inayokufa kutokana na Ugonjwa huo
Naye Pili Lameck Ndimila Diwani viti maalumu kupitia chama cha Mapinduzi ccm amesema kuwa idara ijipange kuwashawishi wafungaji kuitikia zoezi hilo na siyo kutumia Lugha chafu na Vitisho kwa Wafungaji
Akitoa Ufafanuzi wa zoezi hilo baada ya Madiwani kuchangia hoja, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Maisha Mtipa amesema ushauri wote uliotolewa na Madiwani utazingatiwa ili kufanikisha zoezi la Chanjo ya Mifugo
Akitoa Salamu za chama Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Maswa Ndugu Onesmo Makota amesema kila Diwani awajibike kwenye Oneo lake ili kuleta Maendeleo kwa Wananchi huku akisisitiza madiwani kuhamasisha Wafugaji kujitokeza katika zoezi la Uchanjaji wa mifugo