Sibuka FM

Msimu wa ununuzi wa pamba  2024/2025  Wazinduliwa rasmi  Maswa

15 May 2024, 8:57 pm

Mkuu wa Wilaya ya Maswa (aliyesimama) akiongea na Wadau wa Pamba (hawapo pichani) katika Ukumbi wa Halmashauri ya Maswa Wakati wa Uzinduzi wa Ununuzi wa Zao la Pamba kwa Msimu wa 2024/ 2025, Kulia kwake ni Ally Mabrouk Mwakilishi Bodi ya Pamba Maswa, Kushoto kwake ni Maisha Mtipa DED Maswa na wa Mwisho kushoto ni Robert Urasa- Daico Maswa. Picha Na Nicholaus Machunda

Mkuu wa Wilaya ya Maswa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mazao amezindua msimu wa ununuzi wa pamba 2024/2025 Wilayani hapa na kuzitaka kampuni zote zinayodaiwa ushuru wa musimu uliopita hazitaruhusiwa kuanza kununua kabla ya kulipa madeni yao.

Msimu  wa  Ununuzi  wa  zao  la  pamba ( dhahabu  nyeupe) 2024/ 2025 wilayani Maswa  umezinduliwa  rasmi  na  Mkuu  wa  Wilaya  Mhe  Aswege  Kaminyoge   na  kuwataka  wanunuzi  wa  zao  hilo kuweka  utaratibu  mzuri  usiokuwa  na maswali  na manung’uniko kwa  pande  zote.

Mh  Kaminyoge  ambaye  pia  ni  Mwenyekiti  wa  Kamati ya  Mazao  Wilayani  hapa  amesema  kuwa  kabla  hawajaanza  kununua rasmi   Wakae  kwa  Pamoja  na  Wadau wengine  wa  Pamba  ili kuweka  sawa namna  ya  ulipaji wa  Fedha  kutoka  kwa  Kampuni  za  Ununuzi  kwenda  kwa  Amcos  na  kutoka  kwa  Amcos  kwenda  kwa  Wakulima

Sauti ya DC Maswa Aswege Kaminyoge wakati wa Ufunguzi wa Msimu wa Pamba

Mwakilishi  wa  Bodi  ya  Pamba  Wilayani  Maswa  Ally  Mabrouk  ametoa utaratibu  wa  kampuni  ipi  itanunua  maeneo gani  na  Kuwataka   kufuata  Utaratibu  uliowekwa  na  Bodi  ya  Pamba   na  Kampuni itakayokiuka  Mashariti  ya  Ununuzi ,  Pamba  yake  itataifishwa  na  Serikali pamoja  na  Kufutiwa Leseni

Sauti ya Ally Mabrouk- Bodi ya Pamba Maswa

Maisha  Mtipa   ni  Mkurugenzi  Mtendaji  wa  Halmashauri  ya  Wilaya  ya  Maswa  ameshauri kampuni  za  Ununuzi  kuangalia  Usalama  wa  Fedha  zao  wanazowekeza  kwenye  Amcos ili  wanunuliwa  Pamba na  siyo  kukimbilia kununua  tu  bila  kuweka   Makubaliano  Mazuri  kati  ya  Kampuni ya Ununuzi  na  Amcos

Sauti ya Maisha Mtipa – DED Maswa

Kwa  Upande  wake  Meneja  wa  Chama  Kikuu  cha  Ushirika Mkoani  Simiyu   Ndugu  Falesi  Muganda  ametoa  rai  kwa   Viongozi   wa   Vyama  vya  Ushirika (Amcos ) wanapaswa  kuwa  Wazalendo  na Waadilifu  kwani  wanajukumu  kubwa  la  Kuwasaidia  Wakuima  na   siyo  kuwaibia.

Sauti ya Fales Muganda – Meneja SIMCU

Akitoa  taarifa  ya  utekelezaji  wa  shughuli  za  kilimo  cha  Pamba , Mkuu  wa  Idara  ya  Kilimo, Mifugo  na  Uvuvi   Robert  Urasa  amesema  kuwa  Malengo  ya  Uzalishaji  yameshindwa  kufikiwa  kutokana  na  Mvua  zilizonyesha  juu  ya  Wastani zilipelekea  baadhi ya  kulima  Kushindwa  kulima  Zao  hilo

Sauti ya Robert Urasa – Daico Maswa

Naye  Meneja  Wakala  wa  vipimo    Mkoa  wa  Simiyu  Francis  Olwero  amewataka  Viongozi  wa  Amcos  kupeleka  Mizao  yote  kwenda  kuhakikiwa  na  kuwekewa  Mhuri  kwa  ajili  ya  kutumika  katika  Ununuzi  wa  Zao  la  Pamba  na  Wasikubali  kutumia  Mizani  ambayo  haijahakikiwa  na  Wakala  wa  Vipimo  kwani  watakuwa  wanaingia  kwenye  Mgogoro  na  Serikali

Sauti ya Francis Olwero – Meneja Wakala wa Vipimo Simiyu
Wadau wa Pamba wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya (hayupo pichani) Wakati wa Uzinduzi wa Msimu wa Ununuzi wa Pamba 2024/ 2025