DC Maswa akabidhi pikipiki kwa CBWSOs
7 May 2024, 7:54 pm
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh. Aswege Kaminyoge amewataka viongozi wa CBWSOs zilizogawiwa pikipiki kuzitumia katika malengo yaliyokusudiwa ili kuleta mabadiliko katika utoaji wa huduma za maji na siyo shughuli binafsi zisizo na tija.
Na Nicholaus Machunda
Mkuu wa Wilaya ya Maswa, mkoani Simiyu Mhe, Aswege Kaminyoge amekabidhi pikipiki nne aina ya TVS zenye thamani ya shiilingi milioni kumi na sita kwa ajili ya kurahisisha shughuli za Jumuiya ya Watoa huduma ya Maji ngazi ya Jamii (CBWSOs) kupitia Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini – RUWASA Wilayani Maswa
Akikabidhi pikipiki kwa Viongozi wa Jumuiya za Watoa Huduma za Maji, Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa lengo la pikipiki hizo ni kwenda kusaidia Jamii husika katika kutatua changamoto kwenye Utoaji wa huduma za Maji na siyo kuzifanyia Shughuli binafsi
Mhe, Kaminyoge ameongeza kuwa Mhe Rais Samia ametoa fedha nyingi katika Wilaya ya Maswa ambapo Miradi Mikubwa ya Maji kila vijiji na kata inaendelea kutekelezwa na kutoa Wito kwa Meneja RUWASA Wilayani hapa kuwasimamia kikamilifu Wakandarasi Wakamilishe kwa Wakati ili kupunguza Adha ya Maji
Mhandisi Lucas Madaha ni Meneja Ruwasa Wilayani Maswa amesema kuwa Wamejikita kuziwezesha CBWSOs katika Utekelezaji wa Majukumu yake kwa Wananchi na kuongeza Upatikanaji wa Huduma za Maji Vijijini
Akitoa Taarifa ya Utekelezaji wa Miradi ya Maji na Ununuzi wa Pikipiki Afisa Maendeleo ya Jamii wa RUWASA Wilayani hapa ndugu Willison Magaigwa amesema kuwa kwa Sasa upatikanaji wa Maji umeongezeka kutoka Asilimia 68.9% hadi kufikia Asilimia 74.6% kwa Sasa huku akitaja changamoto zinazowakabili Jumuiya za Watoa Huduma za Maji
Kwa Upande wake Mkandarasi anayetekeleza Miradi ya Maji Wilaya hapa amesema kuwa anamshukuru Rais Samia kwa kutoa tenda kwa Kampuni za Wazawa hivyo kuahidi kukamilisha kwa Wakati ili Wananchi Wanufaike na Miradi hiyo
Steven Fabiani Biseko ni miongoni mwa Viongozi wa CBWSOs waliokabidhiwa Pikipiki amesema kuwa Watazitunza na kuzitumia kwa Manufaa ya Taasisi na siyo binafsi ili zilete Mabadiliko katika utoaji wa Huduma za Maji Vijijini