Sibuka FM

Maswa queens na Raha queens hakuna mbabe Simiyu

6 May 2024, 5:49 pm

Picha ya pamoja ya wachezaji wa Maswa warriors queens tayari Kwa mechi ya mabingwa mkoa Picha na Paul Yohana

Utamu wa ligi ya wanawake Simiyu wafikia pazuri huku vipaji  vya mpira wa miguu kwa wanawake vikiibuliwa na kupelekea wazazi na walezi wa vijana wa kike kuhamasisha mabinti zao kucheza mpira wa miguu

Na,Paul Yohana

Fainali ya kwanza  ligi ya mabingwa wanawake mkoa wa Simiyu imefanyika katika uwanja wa nguzo nane  maswa  kati ya Maswa warriors queens ya Maswa na Raha queens ya Baraiadi na kuhushudia mchezo huo ukimalizika kwa sare ya bila kufungana

Kocha mkuu wa Maswa warriors, Shaban  Kalinga amesema kuwa  mwisho wa mchezo huo ndio mwanzo wa mchezo unaofuta na magoli popote yanapatikana.

Sauti ya kocha wa Maswa warriors queens

Husna  Salum ni timu kapteni wa Maswa warrios  amekubali matokeo ya mchezo wa kwanza lakini ana imani na mechi ya marudianokuwa  watafanya vizuri zaidi

Sauti ya timu kapteni wa Maswa warriors queens

Akizungumza na Sibuka sport kocha mkuu wa  Raha quuens, Rajabu Komba amefurahishwa na matokeo ya bila kufungana ugenini akiwa na matumaini makubwa ya kufanya vizuri wakiwa nyumbani katika uwanja wa  halmashauri ya Bariadi

Sauti ya kocha wa Raha queens

Kwa upande wake kapteni wa  Raha queens, Ester Mussa  amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa mpira wa miguu mkoa wa Simiyu hasa wakazi wa Bariadi wasiwe na shaka kwani watafanya vizuri katika mchezo wa marudiano na kuibuka mabingwa mkoa.

Sauti ya timu kapteni wa Raha queens

Fainali ya pili itapigwa  mei ,12/2024 katika uwanja wa halmashauri ya mji wa Bariadi ambapo mshindi ataenda kuwakilisha mkoa katika mashindano ya mabingwa wa mikoa kwa mpira wa miguu upande wa  wanawake