Maswa wanogesha muungano kwa kutoa madawati
24 April 2024, 10:46 am
Wakuu wa Idara Halmashauri ya Wilaya ya Maswa wamekabidhi Seti za Madawati Miatatu kwa ajili ya Shule za Msingi na Sekondari ili kupunguza Uhaba unaozikabiri shule hizo baada ya kujibana kwenye Bajeti za Matumizi ya Ofisi zao
Na Nicholaus Machunda
Katika Kusherekea Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Wakuu wa Idara katika Halmashauri ya Wilaya ya Maswa iliyopo Mkoani Simiyu Wameadhimisha kwa Kutoa Madawati kwa Shule za Msingi na Sekondaari yenye thamani ya Shilingi Milioni 18.
Akikabidhi seti hizo za Madawati kwa Baadhi ya Wakuu wa Shule za Msingi na Sekondari, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mhe Aswege Kaminyoge amesema kuwa Madawati yanaenda kupunguza Uhaba wa Samani na kusisitiza kuyatunza ili yadumu kwa ajili ya kizazi kijacho
Mh Kaminyoge amewapongeza Wakuu wa Idara hao kwa kujibana katika bajeti za Ofisi zao na kununua Madawati na Kutoa Wito kwa Taasisi zingine kwenye Ofisi zao kutenga Bajeti ili kurudisha shukurani kwa Jamii kuchangia Miundo mbinu mingine kama Madawati ili kufanya wanafunzi wasome bila shida yoyote..
Akimkaribisha Mkuu wa Wilaya, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Ardhi Ndugu Vivian Christian amesema kuwa Madawati hayo yanaenda kupunguza changamoto ya uhaba wa Madawati kwa baadhi ya Shule
Mwl Fedelis Apolinary ni Afisa Elimu Sekondari Wilayani hapa amesema idara yake imepata Madawati Mia mbili ambapo yatapelekwa katika Shule za Sekondari Nyongo na Sayusayu ambazo zilibainika kuwa na Uhaba Mkubwa huku akiahidi awamu nyingine kupeleka katika shule zingine.
Akitoa Ufafanuzi wa Utengenezaji wa Madawati hayo, Mkuu wa Chuo cha Ufundi Stadi Binza Mwalimu Mabula Skampamu Daniel amesema Madawati hayo wameyatengeneza kwa Ubora wa hali ya Juu hivyo yatadumu kwa Muda Mrefu huku akitoa Rai kwa Wadau na Taasisi mbalimbali kujitokeza kutengeneza ili kusaidia Wanafunzi .