CHADEMA Simiyu yajipanga kuingia kwa kishindo uchaguzi serikali za mitaa
25 February 2024, 6:14 pm
Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Simiyu kimesema kuwa kimejipanga kuingia kwa kishindo katika uchaguzi wa serikali za mitaa utaofanyika mwishoni mwa mwaka huu wa 2024.
Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mkoa wa Simiyu Musa Onesmo wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uamuzi wa chama hicho kushiriki katika chaguzi zijazo za serikali.
Aidha Mwenyekiti huyo wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Mkoa wa Simiyu amewahamasisha Wanachama na Wananchi ujitokeza kwa Wingi kushiriki Maandamano ya Amani hivyo Wajiandae kupokea Maandamo Mkoani hapa.
Onesmo amesema kuwa Kupanda kwa gharama za Maisha kunapelekea Ugumu wa Maisha kwa Wananchi hasa kwa Bidhaa Muhimu ikiwemo Sukari ambapo kuipata hadi Upange Foleni au kuuziwa kwa Kufahamiana.