Sibuka FM

ugumu wa maisha chanzo kudorora kwa sikukuu za mwisho wa mwaka maswa

26 December 2023, 6:16 pm

Pichani ni hali ya soko kuu mjini Maswa inavyoonekana likiwa patupu hali ya kwamba ni maandalizi ya sikukuu za mwisho wa mwaka Picha na Alex Sayi

Sikukuu za mwisho wa mwaka zimepoteza mwamko kwa Wananchi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha ya kila hivyo kukosa fedha za ziada kwa ajili ya kugharamia sherehe hizo

Na Alex Sayi-Simiyu

Imebainishwa kuwa mabadiliko ya tabia ya Nchi na ugumu wa maisha vimeendelea kuchangia kupokelewa kwa unyonge Siku Kuu za Mwisho wa Mwaka (Krismasi na Mwaka Mpya.

Hayo yamesemwa na baadhi ya Wananchi na Wakazi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wakati wakitoa maoni yao kuhusiana na kudorora kwa Siku Kuu za Mwisho wa Mwaka Mkaoni Hapa.

WAFANYA BIASHARA WA SOKO KUU MASWA.

Akizungumza na Sibuka fm Mwenyekiti wa Soko kuu Mjini Maswa Bw,Naftali Joram amesema kuwa hali ya kibiashara Sokoni hapo imedorora kutokana na kukosa mwitikio wa wananchi kwenye kuelekea Siku Kuu hizo za Mwisho wa Mwaka ikilinganishwa na Mwaka jana

Akizungumzia bei ya Bidhaa Sokoni hapo Mwenyekiti huyo amesema kuwa Bei ya Sukari imepanda zaidi Mwaka huu ikilinganishwa na Mwaka jana.

“Sukari kwa sasa imepanda sana ambapo tunanunua kwa bei ya jumla jumla mfuko wa kg 25 kwa bei ya Tsh.74,000/= hali ambayo inatufanya tuuze kwa Tsh.3500 kwa Kg 1 ambapo kwa mwaka jana kg 1 ya Sukari iliuzwa kwa Tsh.2800 hadi 300″‘.Amesema Naftari

Ameongeza kuwa Bei ya Mchele Kg(1)kwa  sasa inanunuliwa kwa Sh.2,000/=hadi Sh.2,200/=ali hali mwaka jana ilinunuliwa kwa Sh.2,800/=hadi Sh.3,200/=Maharagwe yakinunuliwa kwa Sh.2,800/=hadi Sh.3,000/=sawa na Mwaka jana,Mafuta yakinunuliwa kwa Sh.5,000/=Lt(1)ili hali Mwaka jana yakinunuliwa kwa Sh.6,000/=hadiSh.7,000/=kwa Lt(1)na Viazi Mviringo vikinunuliwa kwa Bei ya Sh.1,000/=kwa Kg(1)ili hali  Mwaka  jana vikinunuliwa kwa Sh.1,200/=kwa Kg(1).huku Nyama ikiuzwa Sh.8,000/=kwa Kg(1)sawa na Mwaka jana.

Akizungumzia suala la kupanda kwa Bei ya Nyanya na Vitunguu Sokoni hapo Bi.Anna Frank amesema kuwa hiyo imetokana na namna wanavyolangua bidhaa hiyo kwa sasa Debe la Nyanya wanalangua kwa Sh.20,000/=elfu ishirini na Vitunguu wakilangua kwa Sh.30,000/=elfu thelathini kwa Debe.

Daniel Joseph Manyanga Mfanyabiashara wa Duka Wilayani hapa amesema kuwa kupanda kwa gharama ya Bidhaa kumechangia kudorora kwa Sherehe hizi huku akibainisha kuwa kwa sasa Kret ya Soda inanunuliwa kwa Sh.12,000/=hivyo kuwalazimu kuuza Soda(1)Sh.700/=

“Hali ni ngumu vitu vimepanda bei kwa sasa Kreti la Soda tunanunua kwa Sh.12,000/=ali hali awali tulikuwa tunanunua kwa Sh.11,800/=hali hii inatulazimu kuuza Soda (1)Sh.700/=Sukari nayo imepanda Mfuko wa Kg 25 kwa sasa tunaununua kwa Sh.74,000/=natunauza kwa Sh.3,500/ kwa kg 1=”.Amesema Manyanga.

WAFANYABIASHARA WA KUKU NA MBUZI MJIMI MASWA.

Akizungumza na Sibuka Fm  Jila Jagadi mfanyabiashara wa Mbuzi amesema kuwa kwa sasa biashara ya Mbuzi imekuwa ngumu kutokana na Bei ya Mbuzi kwa sasa inayonunuliwa kwa wastani wa SH.150,000/=hadi Sh.180,000/=huku Bei ya Sh.100,000/=kushuka chini wakiuziwa watoto wa Mbuzi.

“Kiukweli Biashara ya Mbuzi imekuwa ngumu tumelazimika kurudi kwenye Kondoo wao angalau Bei yao haijapanda sana,Bei ya Mbuzi iko juu mno na imesababishwa na walanguzi kutoka Silali wananunua hadi vitoto vya Mbuzi kwa Bei ya juu kuanzia Sh.70,000/= nakuendelea”. Amesema Mfanyabiashara huyo

Babu Mjukuu mfanya bishara wa Kuku Mjini hapa amesema kuwa biashara ya Kuku bado imedorora na wateja niwachache na hakuna amsha amsha kama mwaka jana.

“Kwenye banda langu hapa Kuku wakuweza kula anaanzia Sh.15,000/=(Jike)Majogoo ni Sh.18,000/=nakuendelea tunauza hivi kutokana na tunavyowalangua kutoka kwa wafanyabishara wanaowafuata huko vijiji na hii Bei nisawa tu na Mwaka Jana na tuliuza lakini mwaka huu doh,naona hali imepoa sana.”Amesema Mjukuu.

WAFANYABIASHARA WA NGUO NA MAFUNDI NGUO MJINI MASWA.

Akizungumza na Sibuka Fm Mama Alex Mfanyabiashara wa Nguo Mjini hapa amesema kuwa hali ya Biashara kwa msimu huu wa Siku Kuu haijachangamka ikilinganishwa na Msimu wa Mwaka jana.

“Hapa kama unavyoona  Nguo haziendi hakuna wateja kabisa hata Nguo za watoto nazo haziendi na Bei zipo kawaida sana kuanzia Sh.18,000/=hadi Sh.30,000/= Bei tu sawa na Mwaka jana lakini ndoo kama unavyoona sasa hakuna mteja anayekuja kununua nguo kwa ajili ya  Sikukuu ya Mwaka mpya”.Amesema Mama Alex wa Zackaria Fashion Shop.

Mama Alex ameongeza kuwa walitarajia kuona watumishi wanaanza kufanya shopping ya nguo za watoto kuelekea msimu huu wa Siku Kuu lakini nao  hatuwaoni na wachache wanaofika wakuja kwajili ya maandalizi ya Nguo za wototo kwenda Shule.

Elizabeth Boniphace Fundi Nguo Mjini hapa amesema kuwa kumekuwa na wateja wachache mno wa Nguo za Siku Kuu  kwa msimu huu ikilinganishwa na Mwaka jana ila kazi nyingi ninazopokea  kwa sasa hivi ni sale za Shule kila mteja anaekuja hapa anataka nimshonee sare ya Shule.

 “Kiukweli hali ya Mwaka huu ni Ngumu hapa sijapokea Nguo yoyote ya Siku Kuu kushona kama unavyooona hapa nashona unifomu tu za Shule tofauti na Mwaka jana nilikuwa napokea kazi mchanganyiko”.Amesema Elizabeth Boniphace

MAONI YA WANANCHI NA WASOMI

Akizungumza na Sibuka Fm   Emmanuel Kudema mtumishi mstaafu mkazi wa Kata ya Kidema Wilayani Maswa  amesema kuwa kudorora kwa sikuu hizi kwa miaka ya hivi karibuni kumechangia kwa kiasi kikubwa na mabadiliko ya tabia ya Nchi na Ugumu wa maisha.

“Kiukweli ugumu wa maisha unachangia sana lakini pia Wananchi sasa wamekuwa na mwamko wa kusomesha zaidi hivyo badala ya kujicha Kuku mwenye thamani ya Sh.15,000/=hadiSh.20,000/=au Mbuzi wa Sh.150,000/=anaona ni bora kuuza na kugharimia mahitaji ya Watoto Shule”.Amesema Kudema.

Akizungumza na Sibuka Fm  Bunani Bunzari Mwenyekiti wa Tiba Asili Wilaya ya Meatu Mkoani hapa amesema kuwa kwa sasa Wananchi wengi wamekuwa na mwamko wa kusomesha hali inayowafanya wawe wachumi nakubana matumizi yasiyokuwa ya lazima na Bajeti kuelekezwa kwenye kusomesha.

“Kwa sasa kumekuwa na mwamko wa kusomesha ndoo maana unaona hizi Siku Kuu hazipewi kipaumbele sana mtu anapiga hesabu ya fedha inayotumika kugharimia Siku Kuu anaona ni bora aielekeze kwenye shughuli zingine za maendeleo ikiwemo kusomesha”.Amesema Bunani.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Juniors and Child Foundation Joseph Ngeleja Jidayi akizungumzia suala hili amesema kuwa kwa sasa kumekuwa na mwitikio mdogo wa Wananchi kusherehekea Siki Kuu hizi za mwisho wa Mwaka kutoka na ugumu wa maisha,Mfumuko wa Bei na Ubinafsi.

”Kwa sasa hali ni tofauti sana ikilinganishwa na hapo zamani maana tunashuhudia jamii ikizidi kuwa na ubinafsi mno hata Watoto wenye mahitaji maalumu hawapati faraja kutoka kwa jamii inayowazunguka,hawataki kula nao na kujihusisha nao wakiona nimkosi kula nao na wengine kuwa na mitazamo ya imani potofu”.Amesema Jidayi.

Kwa upande wake Jonathan Mnyela Mtaalamu wa Uchumi Tumizi(Applied Economist)Wilayani Maswa  amesema kuwa hali hii ya mdororo  inatokana na hali halisi ya kipato cha kila Raia anachokipata na hasa baada ya matumizi kwenye kipato chake halisi.

”Tunachokiangalia hapa hasa huyu Mwananchi anabakiwa na nini kwenye pato lake halisi baada yakutoa mahitaji yote muhimu ya chakula,kodi ya Nyumba,Kilimo,mahitaji ya Shule ,Usafiri Nk,kisha kinachobaki aweze sasa kukitumia kwenye kusherehekea”.Amesema Mnyela.

 ”Mfumko wa Bei,gharama za maisha zimechangia kwa kiasi kikubwa lakini pia kwa Wakulima wamekuwa waathirika wakubwa zaidi na hata ukiangalia kwa mwaka huu Bei ya Pamba ya Sh.1,060/= tofauti na mwaka jana ambapo pamba ilinunuliwa kwa bei ya Tsh.2100 hivyo imewaathiri sana wakulima hali inayowafanya wasiwe na kipato cha ziada kuweza kugharimia sherehe hizi”.Amesema Mnyela.