Wakulima Maswa waaswa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti
9 August 2023, 4:03 pm
Wakulima Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wahamasishwa kutumia mbegu bora zilizofanyiwa utafiti ili kuongeza uzalishaji kwenye sekta ya kilimo.
Na,Alex Sayi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Maisha Mtipa amewaasa Wakulima Wilayani hapa kutumia mbegu zilizofanyiwa utafiti ili kilimo hicho kiwe na tija kwa Wakulima hao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi huyo kwenye kilele cha siku kuu ya nane nane iliyofanyika maeneo ya Nyakabindi Mkoani Simiyu.
Mkurugenzi huyo ameongeza kwa kumshukuru Rais Samia kwa kuwekeza fedha nyingi kwenye sekta ya Kilimo,huku akiwataka Wanawake na Vijana kujishirikisha na kilimo ili sekta hiyo iwe na tija kwa wakulima hao.
Sauti ya Mkurugenzi wa Halmashauri Maswa Maisha Mtipa.
Mkuu wa Division ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilayani hapa Robert Urasa Alisema kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa inaendelea na mkakati wa kuwahamasisha Wakulima kulima zao la Alzet ambalo nimkombozi kwa Wakulima.
Sauti ya Mkuu wa Divission ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi Wilayani Maswa Robert Urasa
Kwa upande wake Masuka Balele Afisa kilimo wa Campuny ya Advanta toka Mkoani Arusha ambao niwasambazaji wa mbegu hizo Mkoani hapa amewaasa Wakulima,kutumia mbegu hizo kwakuwa zinahimili hali ya hewa Mkaoni Simiyu.
Sauti ya Bwana Shamba toka Kampuny ya Advanta Masuke Balele
Aidha Salome Charles Mkulima mwezeshaji amesema kuwa kilimo cha mbengu za kisasa zilizofanyiwa utafiti zimewasaidia wakulima hao kupata mazao mengi ikilinganishwa na mbengu za kienyeji.