Sibuka Fm: Kongole TADIO, Vikes kwa elimu ya kutangaza kidijitali
10 July 2023, 3:22 pm
Waandishi wa habari wa kituo cha Radio Sibuka Fm wamepatiwa mafunzo ya kuandaa na kutangaza habari za mtandao ili kuendana na kasi ya ushindani wa teknolojia, mafunzo yaliyofanyika katika ofisi za Sibuka Fm zilizopo mjini Maswa mkoani Simiyu.
Na Nicholaus Machunda
Waandishi wa habari wa kituo cha Radio Sibuka Fm wameishukuru Tadio kwa kutoa elimu ya namna ya kutangaza habari kwa njia ya mtandao https://radiotadio.co.tz/sibukafm
Wamesema kuwa kupitia mafunzo hayo sasa watakuwa na uwezo wa kuifikia jamii katika nyanja zote za masafa ya Radio na habari za kwenye mtandao.
Aidha waandishi hao wamesema kuwa wamejifunza namna ya kuweka na kutangaza habari kwenye mtandao na ikawafikia watu wengi zaidi ya kutoka ndani na nje ya masafa ya Radio ili kuendana na ulimwengu wa sasa wa teknolojia.
Hilali Ruhundwa ni mhariri wa Radiotadio amesema kuwa wameamua kuwafuata waandishi kwenye vituo vyao vya Radio ili kuwajengea uwezo wa kujua namna ya kutanaza habari za mtandao ili kuendana na kasi ya dunia.
kuweka na kutangaza habari kwenye mtandao
Ruhundwa amesema kuwa mafunzo hayo yameandaliwa na TADIO kwa Kushirikiana na VIKES yakiwa na lengo la kuhakikisha Radio jamii zinakuwa na uelewa wa kutangaza habari za mtandao kwani kwa sasa dunia ipo huko.