“Changamkieni Fulsa za Udhamini wa Mikopo kutoka PASS TRUST ili Mjikwamue Kiuchumi DC Bariadi Simon Simalenga”
19 April 2023, 5:33 pm
Wananchi Mkoani Simiyu wameaswa kuchangamkia Fulsa za Udhamini wa Mikopo ya hadi Asilimia 80% katika Miradi inayochochea Ukuaji wa Uchumi wa Kijani katika Sekta ya Kilimo, Mifugo na Mazao ya Misitu.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Mh, Simon Simalenga kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Dkt Yahaya Nawanda Wakati Ufunguzi wa Warsha ya kutoa Elimu kuhusu Udhamini wa Mikopo na kampeni ya KIJANISHA MAISHA.
Sauti ya DC Bariadi Simon Simalenga
Langelika Kalebi ni Meneja wa Tasisi ya PASS TRUST Kanda ya Ziwa amesema kuwa Taasisi hiyo imekuwa ikitoa Udhamini wa Mikopo kuanzia Asilimia 20% hadi 60% huku kundi la Wanawake Wanaofanya Miradi inayogusa Uchumi wa Kijani ikifikia hadi Asilimia 80%.
Sauti ya Meneja Pass Trust Kanda ya Ziwa – Langelika Kalebi
Aidha kwa Upande wake Afisa Kilimo Mkoa wa Simiyu Bi Kija Kayenze amesema kuwa Wakulima wengi wa Mkoa wa Simiyu wapo maeneo ya Vijijini hivyo kuitaka Taasisi ya PASS TRUST itumie kila aina ya njia ili kufikisha Elimu hiyo kwa Wakulima ili Wajikwamue Kiuchumi..
Sauti ya Afisa Kilimo Mkoa wa Simiyu – KIJA KAYENZE
Kwa Upande wa Wakulima, Wafugaji na Wafanya Biashara Mkoani hapa Wameishukuru PASS TRUST kwa kuja na njia hiyo ya kuwakomboa kwani mara nyingi wamekuwa wakienda kukopa Fedha kwenye Taasisi za Kifedha na kukosa kutokana ya kushindwa kukidhi vigezo vya kukopesheka.