UZAZI WA MPANGO UNASAIDIA KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI.
29 November 2022, 6:24 pm
Imeelezwa kuwa matumizi ya Uzazi wa Mpango yanasaidia kupunguza kwa asilimia kubwa vifo vitokanavyo na Uzazi kwa akina mama..
Hayo yameelezwa na Dr Boniface Mabonesho Mtaalamu wa Masuala ya Afya ya Uzazi kutoka Zahati ya Mwagala iliyopo Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wakati akizungumza na Radio Sibuka Fm..
Dr Mabonesho amesema kuwa mama anapokuwa na utaratibu wa kuzaa kwa Mpango inasaidia mwanamke kuimarisha Afya yake kabla ya kubeba Ujauzito mwingine..
Amesema kuwa Jamii imekuwa na Mtazamo hasi kuhusu Uzazi wa Mpango “ Jamii imekuwa na Mtazamo hasi kuhusu Uzazi wa Mpango na kuamini kuwa njia hizo zimekuwa zikisababisha Ugumba kwa Wanawake’’
‘’Ni vizuri Jamii ikaelewa kuwa njia za Uzazi wa Mpango hazisababishi Ugumba pengine wanatumia bila kufuata utaratibu na ushauri kutoka kwa madaktari wanapotaka kutumia njia hizo’’
Joyce Masanja ni mama wa watoto wawili kutoka kijiji cha Mwanhonoli kilichopo wilaya ya Maswa amesema kuwa njia za Uzazi zimemsaidia kuzaa watoto kwa kuwapishanisha umri na kuweza kuwahudumia vizuri..
‘’Watoto wangu Anitha na Emmanueli niliwapishanisha kwa muda wa miaka minne(Anita nilimzaa mwaka 2016 mwezi wa 3 na Emmanuel nilimzaa 2020 Mwezi wa 7) hali iliyonipa kuwa na muda mwili kujijenga na kunipa nafasi ya kufanya shughuli zingine za kiuchumi”