MKAKATI WA KUTAMBUA MAMA WAJAWAZITO WOTE KUPITIA DATARI MAALUMU WALETA MATOKEO CHANYA WILAYANI MASWA..
26 September 2022, 11:47 am
Mkakati wa kutambua wajawazito Wilayani Maswa umeleta mabadiliko makubwa ikiligaishwa na hapo awali ambapo wajawazito walikuwa hawatambuliki hali iliyokuwa inapelekea baadhi yao kujifungua majumbani na kuhatarisha Maisha yao.…
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh Aswege Kaminyoge wakati akitoa Elimu kwa Wananchi kupitia Radio Sibuka fm na Kusema kuwa Mkakati huo umekuwa na Manufaa makubwa ya kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi.
“Nipede tu kutoa Ushuhuda kwamba Mkakati tuliokuja nao kama Wilaya ya Maswa kuhakikisha Akina Mama wajawazito wote wanatambuliwa na kuwekwa kwenye Daftari maalumu ili kurahisisha Ufuatiliaji wa Maendeleo ya Ujauzito wao “..
“Mkakati huu umefanya idadi ya Wanaojifungulia kwenye Vituo vya Kutolea Huduma za Afya kuongezeka ikilinganishwa na kipidi kile hatujawa na Mkakati huu ambao lengo lake ni zuri tu na liasaidia sana wataalamu wa Afya kufatilia mwenendo wa mama mjamzito na Changamoto zake “ ..
Akizungumza na Sibuka Fm Radio katika mahojiano maalumu Mratibu wa Huduma ya Afya ya Baba, Mama na Mtoto wilaya ya Maswa Dokta Angella Ngaiza amesema kuwa idadi ya akina mama Wajawazito wanaojifungulia kwenye vituo vya Afya imeongezeka hadi kufikia Asilimia 91.4 % .”
“Kwakweli tuapokea akina mama Wengi sana wanaokuja kujifungulia kwenye Vituo vyetu vya Afya hii nikutokaa na Mkakati tulioanzisha wa kuwa a Daftari Maalumu la kutambua wajawazito Jambo linalotutia Moyo sisi wahudumu “
“ Pia niwashukuru sana Radio Sibuka kwa nafasi mnayotupatia ya Airtime bure kwa ajili ya kuwahabarisha wananchi wetu kuhusu Masuala ya Afya ikiwemo haya ya kujifungulia kweye vituo vya Afya ndio maana idadi imeongezeka sana”