TRA YATOA ELIMU KWA WAFANYA BIASHARA WILAYANI MASWA JUU YA ULIPAJI KODI KWA HIARI.
16 September 2022, 11:10 am
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge amesema kuwa Wananchi wanatakiwa kuwa Wazalendo kwa Kulipa Kodi ya Serikali kwa Maendeleo ya Taifa.
Mh Kaminyoge ametoa wito huo kwenye kikao kati ya Wafanyabiashara wilayani hapo na Maafisa wa Mamlaka ya Mapato TRA chenye lengo la Kujadili Mabadiliko ya Kodi kulingana na Sheria ya Fedha ya Mwaka 2022.
“Nipende tu kusema kwamba Serikali haifanyi Biashara, Serikali inakusaya Kodi kwa ajili ya kazi hizo, sasa jambo kubwa kwa wananchi ni kulipa Kodi na Serikali inarudisha Kodi hizo kwa ajili ya Maendeleo.
Ndio maana TRA wamekuja Kuelimisha ili Sote kwa pamoja tuede katika Mstari mmoja,Kazi yangu kubwa kama mkuu wa Wilaya ni kuhakikisha Usalama, Amani na Utulivu ili nyinyi kufanya kazi pasipo matatizo yoyote”
Mkuu wa Wilaya huyo Amesema kuwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 Wilaya ya Maswa ilipokea Fedha nyingi kwa ajili ya Miradi mbalimbali ya Maendeleo hivyo Kodi wanayotozwa Wananchi ndio inayorudi kwa ajili ya maendeleo..
“Upande wa Afya Mh Rais ameleta Fedha nyingi sana kwa ajili ya Wananchi wake, Katika kipindi kifupi cha Mwaka mmoja Tumejenga vituo vya Afya zaidi ya Vitano nyie wafanyabiashara ni Mashahidi maana hata vifaa vya Ujenzi baadhi tumenunua kwenye Maduka yenu.
Leo hii serikali sisi watu wa Maswa Imetuheshimisha imesema itatutengenezea Barabara ya kutoka Maswa kupitia Lalago, Meatu, Sibiti, Haidom hadi Karatu mkoani Arusha kwa Kiwango cha Lami sasa ni masaa matatu au manne kwenda Arusha hapo hatujataua Mji, hatujafanya Biashara”
Joseph Mtandika ni Meneja Mamlaka ya Mapato- TRA Mkoa wa Simiyu amewapongeza Wananchi wa Mkoa wa Simiyu kwa Kuvuka lengo la Ukusanyaji wa Mapato kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 huku Wilaya ya Maswa ikfikia Asilimia 92% ya Makusanyo yote..
“Niwashuru sana Wana Maswa Mwaka Jana katika Malengo tulikuwa Tukusanye milioni 717 lakini tukaishia kukusanya Asilimia 92, lakini mwaka huu lengo limeongezeka tunatakiwa tukusanye Milioni 940.3 pamoja na mabadiliko ya sheria ya Fedha ndio maana tumekuja hapa kuwakumbusha wajibu wenu wa kulipa Kodi kwa Hiari bila kufukuzana bila kukimbizana ili tuweze kufikia Lengo letu la Milioni 940.3”
Akifungua Kikao hicho Kaimu Mwenyekiti wa Wafanya biashara Wilaya ya Maswa Emmanuel Mlyazenze amesema kuwa Elimu waliyoipata iwasaidie kuwa Waamifu na Wazalendo katika Ulipaji wa Kodi a kuwa Mabalozi kwa Wafanyabiashara wenzao ambao hawakufanikiwa kufika kwenye Kikao hicho.
Baadhi ya Wafanyabiashara Walioshiriki Kikao hicho Wameishukuru TRA kwa Elimu waliyowapatia Juu ya Ulipaji Kodi huku akiwaomba Maafisa wa TRA kujenga Mahusiano Mazuri kwa Wateja wao ili kuleta Ushawishi wa Ulipaji wa Kodi kwa Hiari.
Hapa chini ni picha za matukio mbalimbali ya Kikao cha Wafanyabuiashara na TRA Wilaya ya Maswa.