WANANCHI WA IKUNGU WILAYANI MASWA WAJITOLEA KUJENGA ZAHANATI KUPUNGUZA VIFO VITOKANAVYO NA UZAZI..
22 August 2022, 2:47 pm
Wananchi wa Kijiji cha Ikungu kilichopo kata ya Badi Wilayani Maswa Mkoani Simiyu wamejitolea kujenga Zahanati ili kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi na kusaidia upatikanaji wa Huduma za Afya kijijini hapo..
Wananchi hao wameamua kuchangishana michango kwa kila Kaya ili kujenga zahanati hiyo kutokana na Umbali mrefu wanaopata wa kufuata huduma za Afya vijiji vingine hali inayopelekea kuhatarisha Maisha ya Wakazi wa Eneo hilo
Akizungumza na Sibuka Fm baada ya kutembelewa Mtendaji wa Kijiji hicho cha Ikungu Ndugu Ibrahimu Japheti Lugwasha amesema kuwa wamefikia hatua hiyo baada ya Changamoto wanazozipata za kufuata huduma Umbali mrefu..
Amesema kuwa Akina mama wajawazito wamekuwa wakipata shida hasa inapofika wakati wa Kujifungua hali inayopelekea Wengine kujifungulia njiani na wengine kupoteza Maisha..
Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi Mh Mashimba Ndaki amewatembelea na Kushiriki Ujenzi wa Zahanati hiyo iliyopo Jimboni kwake na kuwataka wajenge mpaka hatua ya Boma halafu yeye atawasaidia Mbao na Bati na vifaa vingine vya kuezekea kwa ajili ya kukamilisha..
Mh Ndaki amesema kukamilika kwa Zahanati hiyo itakuwa Msaada mkubwa kwa wananchi wa Kijiji cha Ikungu na maeneo jirani yanayo yanayozunguka kijiji hicho kwani watapata Huduma kwa Ukaribu …
Nao Baadhi ya wananchi wamemshukuru Mbunge wao kukubali kuwasaidia Kuezeka baada ya Nguvu za wananchi kukamilisha Boma ili kuondoa changamoto hiyo iliyokuwa inapelekea akina Mama Wajawazito kupoteza Maisha wakiwa njiani kufuata huduma za Afya..
Hapa chini ni picha mbalimbali za Mbuge na wanachi wa kijiji cha Ikungu wakishiriki kusomba Tofauti kwa ajili ya kuanzisha Msingi wa Jengo la Zahati kwa nguvu za wananchi..