DC MASWA AOKOA ZAIDI YA LITA 30,000 ZA MAFUTA YA DIESELI ZILIZOTAKA KUIBIWA KATIKA MRADI WA SGR KITUO CHA MALAMPAKA
6 August 2022, 7:44 pm
Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu Aswege Kaminyoge ameliagiza Jeshi la Polisi kuwasaka na kuwakamata watu wote waliofanya hujuma za kutaka kuiba Mafuta aina ya Dieseli katika kituo cha Malampaka ambapo Ujenzi wa Reli ya Kisasa SGR Unaendelea.
Mh Kaminyoge ametoa maagizo baada ya kushtukia mchezo wa Wizi wa Mafuta hayo, ambapo Gari aina ya Scania lenye Namba za Usajili T 766 DJD Mali ya Kampuni ya Ochele Service Station (OSS) Yenye Makao makao makuu yake Wilayani Rorya Mkoani Mara iliyokutwa mita Chache kutoka Eneo la Sehemu ambapo kuna kisima cha Mafuta yanayotuka katika Ujenzi huo..
Asema Gari hilo lilikamatwa Majira ya Saa 4 Usiku August 4 Mwaka huu baada ya Walinzi wa Reli katika Eneo la kupondea Kokoto kuwakurupusha huku milango yote mageti ya kisima cha mafuta hayo ikiwa wazi tayari kwa kwenda kuiba..
Aidha Mh Kaminyoge akatoka Masaa 48 Mmiliki wa Lori hilo na Dreva wake wakamatwa na kufikishwa kwenye Vyombo vya Sheria pamoja na Msimamizi wa Kisima hicho cha Mafuta na Walinzi wote ili iwe fundisho kwa wengine wenye Tabia kama hiyo ya kuihujumu Serikali..