Mkuu wa mkoa wa Simiyu ashangazwa na wahitimu wa (JWTZ) kushindwa kujitegemea.
18 October 2021, 1:30 pm
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh,David Kafulila ameshangazwa na kitendo cha wahitimu wa wafunzo ya (JWTZ)kushindwa kujitegemea baada ya kuhitimu mafunzo yao licha ya Serikali kutumia gharama kubwa kwa ajili ya mafuzo hayo
David Kafulila ameyasema hayo wakati wa kongamano la vijana lilililofanyika Mkoani hapo kwenye ukumbi wa Alliance,kongamano lililoandaliwa na vijana wa vyuo vikuu na wahitimu wa vyuo mkoani hapo (Simiyu Youth Platform) akizungumzia suala hilo mkuu huyo wa Mkoa amewakumbusha vijana falisafa ya misingi ya elimu ya kujitegemea
Kwa upande wake afisa wa maendeleo Mkoani hapa Bw,Fadhili Wiliam,amewakumbusha vijana kuchangamkia fursa ya mikopo ya asilimia 10% inayotolewa na Halmashauri,mikopo ambayo kwa sasa haina riba kwa mujibu wa marekebisho ya sheria ya mikopo hiyo ya mwaka 2018-2019 inayowataka wakurugenzi kutenga 10% ya mapato kwenye Halmashauri zao.
Akizungumza na kongamano hilo kamishina wa vyuo na vyuo vikuu Nchini Bw,Sospiter Bulugu,amewakumbusha vijana kujali afya zao na kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya na vileo ili waweze kuzifikia ndoto zao.