RC Kafulila awahakikishia wakazi wa kijiji cha Malampaka kutatua Kero zao.
16 July 2021, 1:37 pm
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh David Kafulila amewahakikishia wananchi wa Malampaka na mkoa wa Simiyu kutatua Kero zote zinazowakabili ili kuendana na kasi ya Rais wa awamu ya Sita Mh, Samia Suluhu Hasani.
Mh, Kafulila amesema hayo wakati akizungumza na wananchi wa kijiji cha Malampaka kilichopo wilaya ya Maswa mkoa wa Simiyu katika Kampeni yake ya kuzunguka wilaya zote za mkoa ili kusikiliza kero za wananchi na kuzipatia Ufumbuzi..
Aidha Mh Davidi Kafulila amesema kuwa katika kipindi cha siku mia moja za utawala wa Rais Samia Mkoa wa Simiyu Umepokea Fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa Shughuli mbalimbali za maendeleo katika Sekta za Afya, Elimu, Maji, na Miundombinu.
Naye mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya Maswa Ndugu Paul Jidayi amesema kuwa Mkuu wa Mkoa amefanya Jambo jema la kutoka Ofisini kwake na kwenda kusikiliza kero za wananchi hivyo wananchi wawe huru kueleza changamoto zinazowakabiri ili ziweze kufanyiwa kazi .
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh David Kafulila amemuagiza Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa Dokta Fredrick Sagamiko kufuatilia changamoto za Uzembe wa watumishi katika sekta ya Afya wilayani Maswa..
Picha za matukio mbalimbali ya mkutano wa hadhara katika kijiji cha malampaka-Simiyu