Simiyu yazindua Mkakati wa kuongeza Tija katika zao la Pamba.
6 July 2021, 11:57 am
Mkoa wa Simiyu Umezindua Kampeni ya kuongeza Tija katika zao la Pamba ili kuwainua wakulima Kiuchumi.
Kampeni hiyo imezinduliwa na Waziri wa Kilimo Profesa Adolf Mkenda na kusema kuwa Serikali haiwezi kuamua Bei ya Pamba katika Soko la Dunia na Badala yake inauwezo wa kuamua mkulima avune kilo ngapi za Pamba kama atalima kwa Tija.
Profesa Mkenda amesema kuwa ili wakulima wazalishe kwa tija ni lazima kuboresha Upatikanaji wa Mbegu, bora wa mbegu na huduma za Ugani na tayari serikali imetenga Bajeti kwa ajili ya kuwawezesha maafisa Ugani katika utekelezaji wa Majukumu yao..
Akitoa taarifa kwa Waziri wa Kilimo Mkuu wa Wilaya ya Busega Gabriel Zacharia kwa Niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mh, David Kafulila amesema kuwa licha ya mkoa Kuongoza kwa Uzalishaji wa zao la Pamba hapa nchini bado tija katika zao hilo ni ndogo sana ukilinganisha na mataifa mengine yanayolima zao hilo.
Mkurugenzi mkuu Bodi ya Pamba Nchini Ndugu Marco Mtunga amesema kuwa chanzo cha Umasikii kwa wakulima walio wengi ni kilimo cha mazoea chenye tija duni ambacho kinaenda kuisha kupitia kampeni hii..
Naye Balozi wa Pamba katika msimu huu ambae pia ni Mkuu wa Mkoa Msaafu Mh Agrey Mwanri amesema kuwa sasa ni wakati wa kuachana na kilimo cha zamani cha kumwaga mbegu tukutane kwenye Palizi ambacho hakikuwa na Tija kwa wakulima .
Picha za Matukio ya Uzinduzi wa Kampeni ya Kuongeza Tija katika Zao la Pamba mkoani Simiyu