RC Simiyu aagiza kusimamishwa kazi Daktari aliyesababisha kifo cha Mama aliyeenda kujifungua.
24 June 2021, 10:05 am
Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mh David Kafulila amemuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Maswa kumsimamisha kazi mganga Mfawidhi wa Zahati ya Senani iliyopo kata ya Senani wilayani hapa Ally Soud kwa kusababisha Kifo cha Mama na Mtoto aliyeenda kujifungua katika Zahanati hiyo..
Mh, Kafulila ametoa agizo hilo wakati wa Mkutano wa Baraza la Madiwani la kujadili Mapendekezo ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mwaka 2019/2020.
Akielezea tukio hilo Mganga mkuu wa Wilaya ya Maswa Dokta Mpolo Adorati amesema kuwa mama huyo anayejulikana kwa jina la Christina Jilala alifika kwenye Zahanati ya Senani kwa ajili ya kujifungua tarehe 20. 06 mwaka huu lakini hakupata Huduma baada ya Dakitari huyo kwenda kuamushwa na Mhudumu wa Afya ngazi ya Jamii na kumkatalia.
Dokta Mpolo amesema kuwa Kifo hicho kilikuwa kinaepukika endapo mtaalamu huyo angekuwepo katika kituo Chake cha kazi angeona shida hiyo mapema na kutoa taarifa ngazi ya wilaya licha ya mama huyo kuwa na Uzazi Pingamizi.
Katika hatua nyingine mkuu wa mkoa Mh Davidi Kafulila amesema kuwa mkoa umejipanga kuongeza tija ya uzalishaji wa Zao la Pamba kutoka kilo mia mbili kwa Ekari moja kwa sasa hadi kufikia kilo Mia Nane kwa Ekari moja.
Picha mbalimbali.