Wilaya ya Maswa yaadhimisha siku ya mtoto wa Afrika kipekee.
23 June 2021, 9:55 am
Jamii Wilayani Maswa Mkoani Simiyu imeaswa kushirikiana na vyombo vya kisheria katika kuhakikisha inatokomeza ukatili kwa watoto.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa tarafa, tarafa ya Nughu Ndugu Venance Saria kwa niaba ya mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh, Aswege Kaminyoge wakati wa Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika yaliyofanyika katika Uwanja wa CCM- Nguzo Nane Maswa.
Ndugu Saria amesema kuwa hali ya Ukatili kwa watoto kwa wilaya ya Maswa siyo nzuri kulingana na Takwimu zilizopo ambapo amesema kuwa mara nyingi vitendo vya ukatili vimekuwa vikifanywa na watu wa karibu.
Aidha Robert Urasa akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Maswa amesema kuwa katika kutekeza ajenda ya 2040 lazima kila mwananchi ashiriki kwa kutoa Haki kwa watoto ikiwa nipamoja na kuwatimizia Mahitaji yako ya Msingi..
Awali akitoa utanguzi juu ya Maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika Afisa Maendeleo ya Halmashauri ya wilaya ya Maswa Ndugu Rodgers Lyimo amesema kuwa mara nyingi jamii imekuwa ikiwachukulia watoto kama watu wazima kutokana na mwonekano wa maumbo yao.
Kwa Upande wa Wadau mbalimbali wamesisitiza watoto kupewa haki zao zote ili kuondoa unyanyasaji na Ukatili kwani limekuwa tatito kwa jamii.
Kauli mbiu ya Maadhimisho hayo kwa Mwaka huu ni TEKELEZA AGENDA 2040 KWA AFRIKA INAYOLINDA HAKI ZA WATOTO.
-Hapa chini ni picha mbali mbali za matukio ya siku ya Maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika