Waziri Mashimba Ndaki akabidhi viti na Meza Shule za Sekondari kwenye Jimbo lake vyenye thamani ya Mil 18..
18 May 2021, 10:30 am
Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi mkoani Simiyu Mh, Mashimba Ndaki amekabidhi Viti na Meza kwa ajili ya wanafunzi vyenye thamani ya shilingi Milioni Kumi na nane ili kuondoa Changamoto ya Wanafunzi kukaa chini.
Mh, Mashimba amekabidhi viti na Meza hivyo kwa Shule za Sekondari Buchambi, Shishiyu na Nyabubinza kwa niaba ya shule Kumi na nane za Jimbo la Maswa Magharibi.
Waziri Mashimba pia ameahidi kutoa Komputa tano kwa kila shule ya Sekondari zilizopo kwenye Jimbo lake ili wanafunzi waendane na Uimwengu wa Teknolojia..
Awali akitoa taarifa ya Utengenezaji wa Viti na Meza hivyo kwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbuge wa Jimbo la Maswa Magharibiri Mh Mashimba Ndaki, Mkuu wa Wilaya ya Maswa Mh, Aswege Kaminyoge amesema kuwa kwa sasa Shule za Sekondari Jimbo la Maswa Magharibi hazina upungufu mkubwa wa Madawati..
Kwa upande wa Wananchi wa Jimbo la Maswa Magharibi wamemshukuru Mbuge wao kwa Msaada alioutoa wa viti na Meza kwa ajili ya wanafunzi…
Aidha Sibuka Fm imezungumza na wanafunzi ambao ndio walengwa katika msaada huo uliotolewa na Mbuge na kusema kuwa utasaidia kuongeza Ufulu kwa hapo awali walikuwa wakikaa chini.